TANGAZO WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2013 WANATAKIWA KURIPOTI JKT 24/06/2013
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-
1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.
2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.
3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.
5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.
6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.