WATOTO WA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA WAONYESHA VIPAJI VYAO KATIKA MASHINDANO YA UMITASHUMITA
Katika
kuhakikisha kuwa mkoa wa Kagera unarudi katika medani zake za zamani kwenye
michezo, uongozi wa mkoa umeendelea na juhudi mbalimbali za kuendeleza na kuibua vipaji vya watoto katika michezo
mbalimbali ili kuvikuza na kupata
wanamichezo mahili hapo baadae.
Mkoa
wa Kagera umezindua rasmi mashindano ya michezo
kwa shule za msingi (UMITASHUMITA) katika chuo cha Ualimu
Katoke(Muleba) tarehe 05/06/2013 na kuhusisha Halmashauri za Wilaya zote ambazo ni Muleba, Bukoba, Misenyi,
Biharamulo, Karagwe , Kyerwa, Ngara na
Bukoba Manispaa.
Katika
mashindano hayo jumla ya wanafunzi 754 wanashiriki michezo mbalimbali ikiwemo
michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira wa wavu, riadha, mpira wa
netiboli, miruko na mitupo.
Akizindua
mashindano hayo rasmi Afisa Elimu Taaluma Bw. Renatus Bamporiki aliwasistiza
wanamichezo waliofika kushindana na kuonyesha vipaji vyao, kushindana kwa nidhamu kubwa na kuonyesha vipaji ili
viweze kuendelezwa na kuuletea mkoa wa Kagera sifa kama ilivyokuwa zamani pia
na kuwapatia ajira.
Kambi
ya mashindano hayo itachukua siku nne kwa kila Wilaya kuonyeshana ujuzi na
Wilaya zingine. Aidha kati ya wanamichezo 754 watachaguliwa wanamichezo 122
watakowakilisha mkoa katika ngazi ya kanda huko mkoani Kigoma kuanzia tarehe
13/06/2013.
Michezo
hiyo inahusisha pia na wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao wanatoka katika
Manispaa ya Bukoba Mugeza Viziwi, pia kutoka Muleba katika shule za Kaigara na
Rubya. Wanafunzi hao wenyenye mahitaji maalum wanasakata kumbumbu kwelikweli na
kwa ufundi mkubwa sana.
Changamoto,
Vyama vya michezo huo ndiyo ulikuwa wakati mzuri wa kuona vipaji na kuweka
mipango yakuviendeleza lakini hakuna hata kiongozo mmoja anayehudhuria
mashindano hayo. Ili mkoa usonge mbale, viongozi wanahitaji kubadilika
kimtazamo kwa kuanza na watoto wadogo.
Ni
matarajio ya mkoa kuwa watoto watakaochaguliwa katika mashindano hayo wataweza
kuipeperusha bendera ya mkoa wa Kagera vizuri kuanzia ngazi ya mkoa, Kanda na
Taifa.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013