WAZO LA KUFIKIRISHA KUTOKA KWA MWANAKIJIJI
Kama baadhi ya wasanii wetu nyota wanalazimika kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya au kutumia madawa hayo tunaweza kusema kuwa kazi yao ya usanii hailipi licha ya kazi nzuri ambazo baadhi yao wamekuwa wakitoa? Msanii ambaye kazi zake (filamu, muziki n.k) inavuma na kununulika au kuuzika kwanini asiwe na uhakika wa maisha yake hadi kulazimika kutafuta njia nyingine za mkato? Je inawezekana pia utamaduni wa 'hip hop' tayari umeshajikita kwenye bongo flava vile vile ambapo madawa ya kulevya ni sehemu yake hasa hapa Marekani ambapo Hip Hop imeasisiwa? Na kuwa wasanii wetu wanafuata upepo tu wa utamaduni huu? Je, itashangaza kama tutaanza kusikia matumizi ya silaha (firearms) kuhusiana na wasanii wetu - palipo madawa ya kulevya kuna matumizi ya silaha?
Je kama jamii tunao wajibu wowote kuwasaidia vijana hawa au inabidi kuanza kuangalia kwa ukaribu tasnia hii isije ikazidi kuwaharibu watoto wetu ambao wanaona maisha ya "bling bling' yanawezekana bila kujua kuwa yanakuja na gharama kubwa ya maisha? Vipi upande mwingine mimba zisizotarajiwa kwa mabinti ambao wanahusiana na kazi hizi ambao nao kwa ajili ya "kupata chochote" inabidi wajiachilie katika 'huruma na hisani' ya wasanii nyota?
Maswali haya yanatupata kutulazimisha kufikiri.