Balozi za EU nchini zinasumbua watanzania kwa upatikanaji wa VISA za Safari!
Watanzania Wanasumbuliwa Sana na balozi za EU hapa nchini!
Juu ya upatikanaji wa VISA za safari
Imebainika kuwa balozi za nchi za ulaya zilizopo hapa nchini,zikiwemo
balozi za Ujerumani,Ubelgiji,Netherland na nyinginezo,
Zimekuwa zikiwasumbua sana raia wa Tanzania wanaohitaji Visa za kusafaria kwenda katika nchi za ulaya.
Pamoja na watanzania wanatimiza masharti yote yanayohitajika katika kuomba Visa lakini balozi hizo zimekuwa bado zikiwawekea vikwazo visivyo
katika sheria za maombi ya Visa.mfano mtanzania anapo omba Visa ubalozini atapeleka barua ya mwaliko na bima,pamoja na benk statment,
barua ya kazini,pay insleep za mishaara.
Heti bado afisa balozi anadai barua ingine itoke kwa mwenyeji kuonyesha
milijuana vipi? na mgeni mtanzania!
Kwa kweli hakuna uhusiano mzuri katika ya raia na maofisa wa visa wa balozi za EU nchini Tanzania.
Watanzania wanapoomba Visa wanasumbuliwa sana sana za ulaya hapa nchini.
Serikali inaweza kuwa na uhusiano mzuri na balozi hizo lakini raia wa Tanzania hawathaminiwi kabisa na balozi za EU hapa tanzania