ENDELEA KUWA NASI KWA MATUKIO YA UJIO WA RAIS OBAMA
Muonekano wa Ikulu Leo.
Rais wa Marekani Barack Obama akifurahia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua nchini Tanzani katika jiji la Dar es salaam
Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda huu katika ratiba yake ya mwisho wa ziara barani Afrika.
Shangwe zikiendelea.

Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi na kisiasa wanaeleza kuwa ziara ya Rais Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.
Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadaye Rais Kikwete amemuongoza Rais Obama kuelekea Ikulu ya Tanzania kwa ajili ya shughuli zingine zilivyopangwa.