Bukobawadau

FAIDA ZA MCHAI CHAI KWA AFYA YAKO

Ni wengi wanaoutumia na kuufahamu mchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu.

Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya . Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.

Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:

- Kinga dhidi ya saratani

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.

-Husaidia umeng’enyaji wa chakula

Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.

Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau