ALICHOKISEMA WILFRED LWAKATARE LEO BAADA YA KESI YAKE KUAIRISHWA MPAKA 22 JULY 2013
KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK LWAKATARE AMEANDIK:'Asubuhi ya leo mahakama ya Mkazi Kisutu nikiwa nimereport.pembeni yangu ni kijana Ludovick Joseph'.
Nimshukuru Mungu kwa siku njema ya leo na kwa ajili ya watanzania wote.
Leo ikiwa ni siku ya case yangu kusikilizwa Mahakama ya Mkazi Kisutu, nimereport pamoja na makamanda walionisindikiza. Case imehairishwa mpaka tarehe 22 July 2013.
Pamoja na hayo,mshitakiwa no.2 Ludovick Joseph ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokukamilika kwa nyaraka za dhamana,hata hivyo dhamana yake iko wazi.
Tukiwa nje ya mahakama,kijana Ludovick ameonekana kuwa mnyonge na kulia sana akilalamika kutojishughulisha kwa ndugu zake(ambao hawakufika mahakamani) kufuatilia dhamana yake.
Nawatakia kazi njema na tusichoke kulitumikia taifa.
Peopleeeeeeeeeeees!