Bukobawadau

Kodi ya Tshs 1,000 kwa mwezi kwa KILA KADI YA SIMU uliyonayo imeanza rasmi tarehe 01 Julai, 2013. Bunge la wananchi na Wawakilishi wa wananchi, wamepitisha kodi hii! Kumbuka, kodi hii hailipwi na kampuni ya simu; inalipwa na wewe mwenye simu! Kampuni ya simu inakusanya kwa niaba ya serikali. Una maoni gani?

Maoni ya Zitto Kabwe.
Kodi ya Tshs 1,000 kwa mwezi kwa KILA KADI YA SIMU uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi na wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii!

Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya kwa niaba ya serikali. 

Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili. Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki... Ni skandali!

Najisikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.
Next Post Previous Post
Bukobawadau