MANDELA ATIMIZA MIAKA 95 LEO
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
.
SHEREHE ya kuzaliwa kwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, zinafanyika leo hafla itakayoambatana na shughuli za kusaidia wasiojiweza ndani ya jamii ulimwenguni kote leo.
Leo Mandela anaadhimisha kutimiza miaka 95 ingawaje bado yuko mahututi katika hospitali mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Watu mbalimbali wa kujitolea watatumia dakika 67 kwa miradi tofauti ya kuboresha maisha, kila dakika ikiwa inasimamia kila mwaka ambao amekuwa akiwatetea watu maishani mwake
.
Hata hivyo, kulazwa kwake hospitalini na pia migogoro ndani ya familia yake imeathiri uchangamfu wa siku ya leo wa kuzaliwa kwake.
Shirika la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 lilitangaza siku ya kuzaliwa kwake Mandela ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Nobel, kuwa ni ya kuadhimishwa kila mwaka kama njia ya kuwahimiza watu kote ulimwenguni kufanya angalau saa moja ya mambo mema.
Watu mashuhuri na pia wanaosifika duniani wamekuwa wakisaidia juhudi hizo za kukumbuka miaka 67 ya juhudi zake Mandela.
Leo watoto katika shule zilizopo Afrika Kusini wataanza kwa kumwimbia mkongwe huyo, huku watu wanaosifika wakijitolea kupiga rangi shule, kuwapatia nguo watoto maskini.
Shule yenye jina lake inatarajiwa kufunguliwa kama kumbukumbu za shujaa huyo. Nchini Amerika, miji 17 pia imepanga kufanya hafla tofauti kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa