Bukobawadau

MANENO KUTOKA KWA MDAU ANASEMA ;'Karibu Kikwete Hapa Kyerwa'

Tunakukaribisha Bwana mkubwa nakaribu sana, naombanisikutajie mafanakio na ahadi ambazo hazijatimizwa hapa kwetu nyumbani, 
Nyegera waitu. 
Kwetu kuna msemo kuwa "ahosanga umukama niho'olamya ".Yaani,unapomkuta mfalme hapo hapondo unatoa lako la moyoni. Basi langu la moyoni ndo hili,

1. Kwetu pamoja na mnyauko kutumaliza bado kahawa zetu zinasafirishwa nje yanchi (Uganda) eti ni maganda ya kahawa, KDCU na Karagwe Estate ambavyo ni maliya wananchi wetu na Mbunge wetu wa chama chako cha ccm ndo kazi yao hiyo.Nadhani wakueleze kwa nini maganda yapelekwe Uganda kama mbolea na tuna uhabawa mboleya?

2. Kwetu tunachaji simu nje ya nchi, ukikutana na Hiace za asubuhi zinazoendampakani usishangae hazina watu bali zinasafirisha simu nje ya nchi ilituendeleee kuwa hewani.

3. Baadhi ya wanyarwanda wamerudi tena wengine wamepewa hifadhi, hilo nadhaninchimbi alishakwambia. 2007 Mbunge wetu alisema umeme utakuwa tayari na helazimetengwa kutoka SIDA, lakini hata nguzo za mwaka wa 70 zile mzungu na STAMICOwalizokuwa wamepata umeme kutoka Murongo kuchimba Tini kyerwa zimeoza
5. TBC taifa kwetu tangu kuisha vitavya Idd Amini haijawahihata kukoroma kwenye redio zetu, hapa ni banange,mlahao na Fadeco + Karagwe.
6 Ujue hii ndo wilaya iliyopo mbali na Dar essalaam kuliko zote lakinihata kununua Cement Uganda au hata mafuta ya taampakatufanye kimagendo.

7. Kwetu bado polisi wanafunga watu "Katankoro"-vunja kidali.Hapo ni kufunga mikono kwa kamba nyuma mpaka viwiko vikutane, hapo tu bodabodaameendesha vibaya! hapana amekosa hela ya kuwapa ili wasimsumbue.

Mzee wetu Karibu tena.
Next Post Previous Post
Bukobawadau