Bukobawadau

MUENDELEZO WA ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo. 
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo 

Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.
 Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo 
 Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete 
 Rais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane.
 Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara 

 Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa 
 Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa
 Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu 
 Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu 
 Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi
Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu 
JK awaonya wanaolinda wahamiaji haramu

RAIS Jakaya Kikwete amesema watendaji wanaotoa vibali kwa wahamiaji haramu watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Rais Kikwete alitoa onyo hilo jana kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Karagwe na Kyerwa alipokuwa akizindua mradi wa umeme vijijini kilowati 33 katika kijiji cha Nyakayanja.

Alisema watakaobainika kujihusisha na vitendo viovu vya kutoa vibali kwa wahamiaji hao kuwafanya kukaa nchini kinyume cha sheria.

“Kuna baadhi ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji wamejigeuza maofisa uhamiaji wa serikali na kutoa vibali kwa wahamiaji… serikali haitasita kuwachukulia hatua; nasema wakome mara moja,” alisema Kikwete.

Aliongeza katika wiki mbili zijazo kutafanyika operesheni katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma ya kurudisha wahamiaji katika nchi zao.

Alisema wahamiaji hao wamekuwa wakihatarisha amani katika mikoa hiyo ambapo vitendo vya ujambazi, wizi wa mifugo na migogoro na mauaji ya kiholela vimekithiri katika mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Rais Kikwete amezindua miradi tisa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi uwanja wa ndege (Bukoba) na kuweka jiwe la msingi jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika KCU Ltd (Bukoba) kuzindua jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na mradi wa maji Mleba.

Miradi mingine kufungua kivuko kipya (Rusumo -Ngara), uzinduzi wa barabara kwa kiwango cha lami Kagoma Lusahunga (Biharamlo), mradi wa umeme vijijini REA (Karagwe), kuweka jiwe la msingi barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami (kilomita 59.1) Kyaka Bugene na ufunguzi wa wilaya mpya ya Kyerwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau