Bukobawadau

Mwanamke na matumizi ya mwili kama silaha…!

Kuna nguo ambazo, mwanamke anapovaa, hawi huru kwani zinamghasi na kumpa hofu na wasiwasi kwa muda wote anapokuwa amezivaa. Kuna nguo za kubana, kuna nguo fupi sana, kuna nguo zenye kuonyesha sana na nyingine ambazo humnyang’anya mvaaji uhuru wake.

Watu wanapozungumzia nguo za namna hiyo, mtu anaweza kukimbilia kwenye dini au kudhani wanaosema hayo wanafikiri kwa mtindo wa mkabala wa zamani sana. Siyo kweli. Nguo hizi fupi sana, za kubana sana na zenye kuonyesha maungo, zinatoa picha kuu moja kuhusu mwanamke.

Kwamba mwanamke ni lazima aonyeshe maungo yake, jamii na hasa wanaume waone alivyoumbika. Kwa hiyo mwanamke ni mwili na mwili huo ni bidhaa, ambayo bila kuoneshwa hadharani jinsi ilivyo, haitapata mnunuzi. Kama siyo kwa kuonesha mwili wake kama bidhaa, basi atauonyesha ili kulipa fidia.
Fidia gani?
Anahisi au kuamini kwamba, kuna eneo kwenye maisha yake ambalo haliko barabara, iwe sura, elimu, kipato, uhusiano na mengine. Lakini kwa sababu amesifiwa kwamba, ana mwili mzuri sana, anajaribu kutumia mwili huo kuziba huo udhaifu ambao anao au ambao ameambiwa anao. Kwa mfano, kama anaamini kwamba, ana mwili mzuri na kalio lililotokelezea, bora autumie mwili huo kuziba huo udhaifu wa sura mbaya!
Kwa kutembea uchi au kwa kuvaa nguo zenye kubana sana, anahisi kwamba, watu wanamsifu kwa mwili ule na hisia hizo humpa nafuu kutoka katika hisia za udhaifu wa yale maeneo aliyoamini kwamba, yana mapungufu.
Nasikitika kusema kwamba, wanawake wote ambao wanatembea nusu uchi au ambao wanavaa nguo zenye kubana hadi inakifu, wana matatizo mahali fulani kwenye maisha yao. Kuna jambo, mambo, matukio au hisia ambazo zinawafanya wajihisi kwamba, wana udhaifu, kwamba hawako kama ilivyotakiwa, kwenye maeneo hayo.

Mwili, ambao waliambiwa ndio kitu pekee kizuri walicho nacho na wakaamini, ndiyo silaha wanayoitumia kujaribu kujilinda na hisia za kutojitosha walizonazo. Kwa sababu ndiyo silaha pekee, huitumia vibaya hadi inawaumiza wenyewe. Ndiyo maana unawakuta wanatembea nusu-uchi wanazomewa, wanashindwa kupanda kwenye gari, wanahangaika wanapokaa chini kwa kujiziba na pengine kubakwa. Lakini bado hawawezi kuacha kuvaa hivyo, kwa sababu, wakiiacha silaha hiyo, wamekwisha.

Wakianza kuvaa nguo ndefu au zisizobana, watashindwa kabisa kufanya chochote kwa sababu hawajiamini katika eneo lingine lolote kwenye maisha yao, isipokuwa miili yao tu. Wanamudu kuendelea kuishi kwa sababu angalau wana huo mwili ambao waliambiwa ni mzuri, basi.
Hata hivyo, kuna wakati hiyo sifa waliyopewa kwamba miiili yao ni mizuri siyo ya kweli, lakini kwa sababu waliamini, huitumia. Unakuta mwanamke kavaa kiguo kifupi, ukimtazama unaweza kwa haraka kudhani ni ndege aliyenyonyolewa manyoya. Kuna mwingine unaweza kukuta amevaa nguo za kubana na kama huna macho mazuri unaweza kudhani umekutana na kifurushi fulani.

Lengo langu siyo kuwakashifu wanawake kwa mavazi yao ambayo ni uchaguzi wao, hapana. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kuna wanawake wengi ambao huvaa nguo wasizozipenda kwa sababu tu ya kujaribu kuziba mwanya wa hisia za udhaifu walionao dhidi yao.
credit jf.
Next Post Previous Post
Bukobawadau