Mwigulu Nchemba;Other things Remain Constant
Vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba TUISOME RASIMU, TUTAFAKARI, TUJADILI, TUTOE MAONI KWA KUITANGULIZA TANZANIA MIOYONI MWETU. SIO KULENGA KULIKOMOA KUNDI FULANI AU UPANDE FULANI WA NCHI. Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:
A) Ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... ktk maeneo yao.