Bukobawadau

Ni kosa kubwa leo hii Kagame kutumia Genocide kama kisingizio cha kusema na kufanya anachotaka

Hadi sasa najiuliza Raisi wa Kagame na baadhi ya mawaziri wake waliwezaje kuropoka maneno waliyosema pale ambapo raisi wa Tanzania aliposhauri Rwanda iongee na wapinzani wa FDLR.

Kuna mtu aliwahi kusema Kagame ana matatizo ya kisaikolojia (pia mental instability), kutokana na namna yake ya ukuzi ikiwa pamoja na kufiwa baba yake mzazi mapema katika maisha yake na kuwa na umbile dogo sana ambalo hakulipenda. Labda ni kweli.

Kwangu mimi naona tatizo kubwa la Kagame ni moja; kwamba anathibitisha kwa kila aina kwamba common sense is not common to everyone - na Kagame lacks common sense in a big way.

Hatukatai kwamba Genocide ya Rwanda was one of the most painful things to ever happen - sawa tu na Holocaust kule Ujererumani, au apartheid brutality kule South Africa. Na pia it was so regrettable Jumuiya ya Kimataifa haikuwasaidia Watusi waliokuwa wanauwawa mapema kama ilivyobidi.

Lakini Kagame hapaswi kutumia Genocide kama right ya kusema anachotaka na kufanya anachotaka, na kudhani Genocide inampa haki ya ku-dictate anachotaka kwa Rwanda na nchi nyingine.

Mwana saikolojia yeyote atakuambia kwamba Kagame anatumia Genocide kama ticket ya kuwa na utawala wa kibabe, kukandamiza upinzani, kuweka watu mahabusu bila sababu, kupiga kelele (tantrums) kila anapokosolewa! Anatumia genocide kujaribu kugenerate guilty feelings kwa wengine na kujifanya yeye ni innocent victim. Kagame aelewe wengi wetu hatudhani yeye ni innocent victim wa genocide.

Yaani ukimgusa tu Kagame - anapiga kelele - Genocide! Genocide! Hamkutusaidia! Hamkusaidia! Msituingilie! Msituingilie! Wewe ni genocide perpetrators sympathizer!

Leo hii huko Rwanda unaweza kufungwa kwa kutaja neno genocide tofauti na Kagame anavyotaka ikumbukwe!

Hizo, kwa kifupi ni tantrums za kitoto mbazo mtu wa umri wa Kagame hapaswi kuzionyesha miaka 20 baada ya Genocide. Kwa ufupi, Kagame anakuwa kama spoilt child ambaye kwa sababu aliumia kidole labda miezi miwili iliyopopita hataki aguswe kwa kisingizio kuwa ana kidonda!

Kwanza tujiulize - hivi ni kweli Tanzania haistahili kusema lolote juu ya suala la amani linayoihusu Rwanda? Je Kagame amesahau kwamba hata chanzo cha Genocide Rwanda ni safari ya raisi wa Rwanda wakati huo akitokea Tanzania kwa madhumuni ya amani? Je Kagame anasahau kwamba kimbilio kubwa la Watsi wakati wa Genocide ilikuwa ni Tanzania - ambayo wakati huo ikafikisha rekodi ya dunia ya kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi kwa wakati mmoja?

Hivi Kagame anafikiri Tanzania inapenda kuwa na wakimbizi toka Rwanda kila baada ya miaka kadhaa? Je amesahau kuwa Tanzania mara nyingi imekubali gharama za kuwa na wakimbizi toka Rwanda, kuwasomesha na hata kuwapa uhuru wa kuwa Watanzania ikiwa tu wataukana uraia wao wa Rwanda? Je amesahau kuwa baadhi ya mawaziri wake na viongozi wake leo hii walisomeshwa bure na Tanzania na sasa wanachangia kuijenga Rwanda? Je, haoni kwamba yote haya yanaipa nafasi Tanzania kutoa ushauri juu ya amani ya kudumu huko Rwanda?

Kama hakupenda ushauri toka kwa JK wa Tanzania, kwa nini asishukuru na kuukataa kidiplomasia? Je mtu anaepiga kelele na kutukana pale anapopewa ushauri unaokubalika na wengine wengi, si dalili kwamba kweli ana matatizo ya kisaikolojia na huenda hata mental instability?

Kagame anapaswa kujua kwamba kwa Tanzania, suala la Wanyarwanda kukimbia nchi yao na kuja Tanzania haliangalii nani huko Rwanda yuko sahihi - Kagame au FDLR. Tanzania inachojali ni kwamba kusitokee machafuko mengine yatakayoumiza raia wa Rwanda na Tanzania- whether Kagame ana sababu za msingi za kuwachukia FDLR au la. Na pia Tanzania inaangalia kwamba kuwe na suluhisho lenye kuzaa matunda. Wanaoumia katika mgogoro wa Kagame na FDLR ni Warwanda wa kawaida, wala si Kagame. Kwanza Kagame hata huko vitani kupigana na FDLR haendi. Anakaa ofisini na kukubali innocent victims waendelee kuumia kwa msimamo wake usio na kichwa wala miguu juu ya FDLR. Machafuko yakitokea Rwanda leo hii, Kagame hatawazuia Wanyarwanda kukimbilia Tanzania ili kuokoa uhai wao.

Si mara zote nakubaliana na sera za JK, lakini kwa hili la Rwanda, ningependa nimshauri JK ampuuze Kagame, na akumbuke kwamba Nyerere wa Tanzania, ilibidi wakati fulani atukanwe na baadhi ya viongozi wa ANC kwa ajili ya kuwashawishi wakubali kuongea na Makaburu. Maongezi hayo ndio yaliyoletelea Afrika Kusini leo hii kujiita Rainbow nation - kwamba inaundwa na weusi, weupe, na wenye rangi mchanganyiko!

Na je, Kagame anasahau kwamba japo maovu ya kutisha yaliyofanywa na wazungu dhidi ya weusi bado kina Mandela walikubali kukaa nao na kuongelea amani? Ukweli ni kwamba wengi wa Makaburu waliowaumiza weusi hadi leo hii wapo mitaani Afrika Kusini - kwa kuwa weusi wa Afrika Kusini wamekubali yaishe. Hiki ndicho kilichompa umaarufu Mandela - kukubali yaishe.

Sasa yeye Kagame ni nani ambaye kwake mambo ni tofauti sana hawezi kukubali yaishe? Je ile Genocide ya Rwanda inauma sana kuliko Holocaust ya Wanazi, kuliko Apartheid ya South Afrika, kuliko UNITA ya Angola, RENAMO, IRA ya Uingereza, nk?

Genocide ilitokea karibu miaka 20 iliyopita - Huenda hata wengi wa wa wapiganaji wa FDLR leo hii hawakushiriki katika genocide - sasa kwa nini Kagame anataka kuhukumu watoto kwa makosa ya baba zao?

Anachofanya Kagame ni sawa na kusema leo hii Wa -Israel wawachukie Wajerumani kwa ajili ya Holocaust. Je Kagame amesahau ilichukua muda mfupi sana kwa Waisrael kutowahukumu Wajerumani wote kwa maovu dhidi yao? Msumbiji wawachukie RENAMO? Uingereza wawachukie IRA, nk?

Ikiwa Kagame ana watu specific katika FDLR ambao anaona wanastahili kufikishwa katika vyombo vya sheria - basi aliweke hilo wazi, kwa kuwa hata ICC inakubaliana nalo. Lakini leo hii, miaka 20 baada ya genocide, kusema kila mtu aliye FDLR ni mbaya na Kagame hawezi kuongea naye juu ya amani - huko ni kuonyesha kwamba Kagame bado ana tatizo kubwa sana na kisaikolojia na ana behave kama a spoilt child ambae hadi leo hajakua.

Ushauri wa bure kwa Kagame - na akitaka anitukane na mimi; Kagame kama una nguvu pigana na umasikini Rwanda, sio kuelekeza nguvu nyingi kwenye vita. Hela nyingi unazotumia katika kampeni dhidi ya FDLR fikiria ikiwa zingeelekezwa kuboresha afya na elimu Rwanda hali ingekuwaje.

Credit JF
Next Post Previous Post
Bukobawadau