Bukobawadau

PICHA YETU YA LEO NA HABARI MBALIMBALI

Picha yetu ya leo mambo ya kitambo, Mara dodoma hotel,wengine kirefu chake Dada Hadja,wengine Dada hayupo.
Mbatia aipa CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza
Kitendo cha Mkiti wa NCCR James Mbatia kukataa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kati ya NCCR na CHADEMA kuongoza halmashauri ya Uvinza yamesababisha CCM kutumia mwanya huo na kutwaa nafasi ya Makamu Mkiti wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkiti uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya vyama vyote vitatu kushindwa kupata theluthi mbili ya kura.

Katika nafasi ya Mkiti vyama vyote vitatu viliweka wagombea ambapo CCM ilipata kura 8 CHADEMA kura 7 na NCCR kura 6.

Nafasi ya Makamu Mkiti mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani na alipita bila kupingwa.

Katika makubaliano ya awali ngazi ya wilaya na mkoa vyama vya NCCR na Chadema vilikubaliana kuachiana nafasi ambapo ilukubaliwa CHADEMA igombee nafasi ya Mkiti na NCCR Makamu Mkiti.

Katika hali ya kushangaza siku ya kurudisha fomu vyama vyote viwili vilirudisha fomu nafasi ya Mkiti na NCCR ikakataa kugombea nafasi ya Makamu Mkiti hivyo mgombea wa CCM akapita bila kupingwa.

Inadaiwa Mkiti wa NCCR James Mbatia ndiye aliingilia kati kuvunja makubaliano ya vyama hivyo na hatimaye ushindi ukawa upande wa CCM

HABARI KUBWA NCHINI UINGELEZA HIVI SASA;watu wanasubiri kwa hamu na ghamu kupata habari za kuzaliwa kwa mwanamfalme mwingine....kwani mkewe Prince William, Kate Middleton anatarajiwa kujifungua mtoto hii leo. Tayari amekimbizwa hospitalini akiwa anaumwa .
Kwa wale Wadau wa Bukoba mnawajua hawa pasiwakichwa, Kuchoto ni Mbaracka Chizi na kulia ni Rama Kachaa ,hivi ndivyo walivyokutwa na camera yetu na hatukujua ni nini walikuwa wanajadili!!
John Terry hayuko salama Chelsea, anasema Jose Mourinho
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kuwa nahodha wkae John Terry hayuko sawa na kwamba atatakiwa kudhihirisha ubora wake katika kikosi cha kwanza ndani ya mkataba wake.
Terry mwenye umri wa miaka 32 alikuwa ni skipper muhimu katika kikosi cha Mourinho kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 na kwasasa amesaliwa na mwaka mmoja ndani ya mkataba wake.
Mourinho amesema
"Hayuko sawa na mwenyewe anajua kuwa hayukoa sawa. Kitu pekee anachojua ni juu ya urafiki wake lakini kiutaalamu hakuna aliye sawa.
Terry akitwaa mataji chini ya Mourinho
Premier League (2): 2004-05, 2005-06
FA Cup (1): 2006-07
Football League Cup (2): 2004-05, 2006-07
FA Community Shield (1): 2005


VIONGOZI WETU EAST AFRICA KUTOKA KUSHOTO NI PAUL KAGAME WA RWANDA, UHURU KENYATTA WA KENYA , NKURUNZIZA WA BURUNDI, MH J.KIKWETE WATANZANIA NA ALIYEKAA NI RAIS WA UGANDA KAGUTTA YOWERI MUSEVENI.
Next Post Previous Post
Bukobawadau