RAIS KIKWETE ATAWAZWA OMUKAMA (CHIFU) WA MISSENYI, AHITIMISHA ZIARA YA KAGERA
Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.**Omukama Kikwete
Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiy
Rais Jakaya Kikwete baada ya kutawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera akiwa na kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo
“tusicheze ngoma siyo yetu, unyago huu hautuhusu sisi tutauana kwa agenda siyo yetu kuna kitu hapa. lakini yote haya ni jitihada wanazo jaribu kufanya kwamba kwa nini tanzania haina matatizo? sasa waliloligundua hapa la dini maana mengine yote yameshindikana, na haya tunayo gombana nayo kwenye dini hayana maelezo yake kwa sababu biblia imebaki kuwa biblia haina ukurasa mpya ulio andikwa leo na quran imebaki quran haina ukurasa mpya ulio andikwa leo na wote hawa wako kwa zaidi ya miaka mia mbili kwanini hawakugombana hapo wanagombana leo, waislam nawasema wakati mwingine wananichukia wakristo nawasema wananichukia nichukieni lakini ntaendelea kuwaambia hili baya”