Bukobawadau

RAIS KIKWETE AWASILI MJINI BUKOBA

Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Bukoba Mhe Anatory Amani

Rais JAKAYA KIKWETE amewasili Mjini BUKOBA tayari kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa inayofanyika kitaifa Mkoani KAGERA hapo kesho.


Baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa BUKOBA , Rais KIKWETE ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa BUKOBA.



Katika hotuba yake fupi kabla ya kuweka jiwe la Msingi Rais KIKWETE Amesema ametimiza ahadi yake kwa kukarabati ujenzi wa uwanja huo

Awali Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali itaendelea na kazi ya kujenga viwanja vya ndege katika baadhi ya mikoa

Mradi wa ukarabati wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa BUKOBA umegharimu zaidi ya shilingi BILIONI 21 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania.
Mradi huo ulioanza February 2012 unatarajiwa kumalizika February Mwakani.

Mh. Rais  Jakaya Kikwete akisalimiana na baba Askofu Kilaini  mara tu alipowasili uwanja wa ndege Mjini Bukoba



·   Aweka Jiwe la Msingi Upanuzi  wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba
·   Azindua Jengo la Kitega Uchumi la Chama cha Ushirika KCU 1990 LTD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amewsili leo 24 Julai, 2013 mkoani Kagera na kuanza rasmi ziara yake ya kikazi.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa  Bukoba  majira ya saa 10: 30 jioni Mhe. Dk. Kikwete aliweka jiwe la msingi katika upanuzi na ukarabati wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Mhe. Dk. Kikwete katika kuweka jiwe la msingi alisema kuwa hizo ni mvua za rasharasha katika juhudi za kukuza sekta ya uchukuzi katika mkoa wa Kagera.
Alisema serikali inakusudia kujenga uwanja wa ndege wa Kimataifa mkoani Kagera Omukajunguti Wilayani Missenyi ili kurahisisha Mawasiliano na kuundeleza mkoa wa Kagera.
Pia Mhe. Dk. Kikwete alisema kuwa uwanja wa ndege wa Bukoba umefanyiwa upanuzi na kuwekewa rami ili wakati wa wa ujenzi wa uwanja mpya wa Omukajunguti utakapoanza kujengwa huduma zisisimame.
Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba utatumia gharama ya zaidi ya shilingi bilioni ishirini na moja mpaka kukamilika kwake na mradi huo ulianza Februari mwaka 2012 na unatarajia kukamilika Februari 2014.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefungua jengo la kitega uchumi la Chama cha Ushirika cha Kagera Cooperative Union 1990 LTD katikati ya mji wa Bukoba.
Mara baada ya kufungua jengo hilo  akiongea na wananchi Mhe. Dk. Kikwete aliwashukuru viongozi wa chama hicho kwa kuwekeza katika maendeleo na vitu vinavyoonekana.
Vilevile aliwasistiza viongozi wa KCU 1990 LTD kuboresha maisha ya wakulima kwa kuongeza thamani ya mazao yao hapa hapa mkoani Kagera ili mkulima anufaike na kilimo cha zao la kahawa.
Aidha Mhe. Kikwete alisema kuwa KCU 1990 LTD ni chama cha mfano nchini na wananchi kutoka sehemu nyinginezo nchini wanapaswa kuja Kagera kujifunza ushirika unavyofanya kazi.
Rais Kikwete ataendelea na ziara yake 25 Julai, 2013 mara baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Kagera katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya Wilayani Muleba na yeye ndiye atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau