Rais wa Sudan Kusini afuta baraza lake la mawaziri.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir jana alifuta baraza lake la mawaziri na kumwondoa makamu rais wake na pia kumsimamisha kazi kiongozi mkuu wa chama tawala.
Hatua hiyo ilitangazwa katika amri Jumanne kati kati ya ripoti kwamba kuna upinzani umejitokeza kati ya viongozi wa Sudan Kusini . Makamu rais aliyetolewa madarakani Rieck Macher amesema atagombea urais 2015.
Barnaba Marial Benjamin ambaye amefukuzwa katika nafasi ya waziri wa habari aliiambia Sauti ya Amerika kwamba uamuzi huo haukuwa wa kushangaza kwa wasudan kusini wengi.