Bukobawadau

Safari Njema na karibu tena Tanzania Barack Obama


Rais wa Marekani Barack Obama ameondoka nchini muda huu kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa M Julius Nyerere huku maelfu ya wananchi wa Tanzania wakijitokeza barabarani kumuaga.
Rais Obama alikuwa nchini katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapoametaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za kielimu kwa  vijana kwa lengo la kuongeza ajira

Jijini Dar es salama Barabara za Ally Hassan Mwinyi, Mandela, Sam Nujoma na ile ya Morogoro zilifungwa kwa muda kuanzia majira ya saa tatu asubuhi huku maelfu ya wananchi wakitanda barabarani kwa lengo la kumuaga rais huyo.
Mara baada ya kufika katika  uwanja wa Ndege Rais Obama na Mkewe walitumia  muda mfupi kuagana na mwenyeji wao Rais Kikwete na mkewe ikiwa ni pamoja na kuwaaga mamia ya viongozi waliofika uwanjani hapo.
fuatana nasi kwa taarifa zaidi
Rais Obama awasili, aisifu Tanzania
Dar es Salaam. Rais Barack wa Marekani, Obama ametaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za vijana kwa lengo la kuongeza ajira.
Kiongozi huyo aliwasili Dar es Salaam jana mchana ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na Senegal na Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati alipozungumza na mwenyeji wake huyo.
Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa mkubwa wa umeme uitwao Power Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.
Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.
Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora. Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.
Next Post Previous Post
Bukobawadau