Bukobawadau

Sherehe London kwa kuzaliwa mwanamfalme

 Ujumbe wa heri njema umeendelea kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.
Mwanamfalme William na mkewe Kate ,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa kwanzaJumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini hajapewa jina.
Katika taarifa fupi William,amesema wana furaha isiyo na kifani.
Baadaye leo jeshi la Uingereza linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40 hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.
Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa mwanamfalme huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na moja ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la Buckingham, zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana kwa Uingereza.
Naye wawiri mkuu wa Australia, Kevin Rudd, alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola, huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William baada ya kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.
SOURCE BBC
Next Post Previous Post
Bukobawadau