TUNAENDELEA KUWATAKIA WAISLAM NYOTE MFUNGO MWEMA WA RAMADHAN;Hadithi ya leo (8)
Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
الصِّيَامُ جُنَّةٌ، فَإِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ صَائِمً
ا فَلَا يَرْفُثْ
وَ
لَا يَجْهَلْ، فَإِنِ امْرُؤٌ قَاتَلَهُ أَوْ شَاتَمَهُ فَلْيَقُلْ إِنِّي صَائِمٌ إِنِّي صَائِمٌ”
Funga ni kinga. Endapo mmoja wenu amefunga asitamke maneno machafu ( matusi na mfano wake) wala asiseme kwa sauti kubwa ( wakati wa kukasirika). Na endapo mtu atataka ugomvi nae au kamtukana basi amwambie, ‘Hakika mimi nimefunga, Hakika mimi nimefunga
Imepokewa na AnNasaaiy
Tunapofunga hatujizuii na kula, kunywa na matamanio ( kustarehe na aila zetu) pekee bali pia hujizuia na mambo mengine kama ugomvi, matusi , kufitinisha na mawazo yoyote ambayo yatatuweka mbali na Allaah Subhaanahu Wata’ala.Ndiyo maana tumepewa suluhisho endapo tutajikuta katika hali hii ni kumjuulisha tu mwenzako kama wewe upo katika funga hivyo haiyumkini kutenda au kunena yaliyo kinyume na maadili ya funga.
Ewe Mola, tuepushe ndimi zetu na matusi na maneno yenye kuudhi, tuepushe nyoyo zetu na kuchukia na kufitinisha. Tuepushe viungo vyetu vyengine kujiepusha na yenye kukuasi wewe Yaa Rabbal ‘Aalamiyn
Aamiyn