Bukobawadau

ZEE LA NYETI : Tichaaaa, kisipoeleweka haina kuwaka! …jipange!

Juzikati wakati nakatiza mitaa ya homu kwa ajili ya mistrechi, nikakutana na washkaji wawili wakanisimamisha, uliza nini? Eti wananiamkia, nikaona kama utani hivi, ...kumbe walikuwa siriasi, wanapiga buku na festi boni wangu bwana...

Nikajishtukia kweli, babaenu, …kumbe nshakuwa mtu mzima, basi tu kafiga kanaruhusu mtu mzima kuonekana yanki lakini kiukweli, niko ejidi sana.

Niaje kwanza wanawani?
Mhola sana?
Haya...
Wenye kunidai komaeni naweza kudedi enetaimu, nshastuka umri ndiyo unasepa hivi, mwanangu mwenyewe Nyaisanga kaamua kwenda kulikita mkoa anajilia bata wake kiulaiiiini, nimebaki mimi tu wa longtaimu napigana vikumbo na watoto, hatukawii kuvunjiana heshima humu, ngoja nijiuzulu hii kazi na madogo nao watanue au siyo?

Mzuka mzito!
Sasa bwana ukiachana na ishu za uzee na mambo mengine babaako kama nina kijistori cha kijinga kabisa kanitumia mwanangu Mahisi, ujue kanipa zipi? Juzikati kuna ticha unaambiwa kampa mbata denti wake mpaka hajitambui kisa eti kaulizwa swali ambalo alishindwa kulijibu, eti la kijinga halina msingi.

Uliza swali gani sasa?

Hahahah, ila dogo naye kwa kweli alikuwa anazingua hata kama mimi ningemaindi lakini nisingemchapa kihiiivyo, ningemtoa nduki tu akapumzike mbele.

Denti bwana kamuibukia ticha nini, ...yuko siriasi yaani akampa zipi ujue?
“Ticha nina swali”.

Maticha sasa si unajua zao? Akajifanya yuko vere siriasi, kimiwani kakishusha nini anamuangalia dogo kwa chini, mwenyewe akahisi analetewa kitu iiiiize si unajua mambo ya praimare? Akapigwa na swali la dagaa!

“Mwalimu eti dagaa kwa Kiingereza wanaitwaje?”

...Usikute hata wewe unayesoma saa hizi huna uhakika na jibu lako.

Ticha unaambiwa alimcheki yule dogooooooo, akahisi kama dogo kadhamiria kumzingua hivi, akaanza kumtoa nduki kudadadeki, nduki mbaya na dogo naye yumo katika kupepea, dizaini ndigo, yuko kama Madenge flani hivi...

Nduki mbayaaaaa!

Stori huko mbele mbele inaendelea lakini mimi najiuliza haukamz ticha kama umeshindwa kitu cha kumjibu denti wako unakuja juu, si unazama gugo tu unakicheki fasta unakijua unamwambia dogo, kwani kuna noma hapo wanangu au ticha alikuwa na jingine jambo?

Manake hawaeleweki jamaa mjue...

Hii ipo sana kwenye jamii zetu na nimeiibua makusudi, watu bwana hawataki kuambiwa kama hawajui ukiuliza unaambiwa huyu mkubwa usimkosoe, wapi kwa wapi bwana?

...timueni huko!
Next Post Previous Post
Bukobawadau