Bukobawadau

Ziara ya Rais Kikwete wilayani muleba

Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
 Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni
 Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka
 Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo

Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria
Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba
Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa maji
Mwananchi mwingine akitwishwa maji

Rais Kikwete akisalimia wananchi
Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba
Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente
Rais Kikwete akifurahia ngoma
Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba
Rais Kikwete akihutubia wana Muleba



Dua ikiombwa baada ya futari

Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo


UMILIKAJI HOLELA WA SILAHA

Rais Jakaya Kikwete ametoa wiki mbili kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha mara moja , kabla ya Oparesheni maalum ya kuanza kuwakamata watu hao, itakayohusisha mikoa ya Kagera, Kigoma Na Geita.

Mikoa hii inatajwa kuwa na matukio mengi ya ujambazi na pia kuwa sehemu kubwa ya upenyezaji wa silaha toka katika nchi jirani.

Inakadiliwa kuwa zaidi ya watu 10 hufariki kila siku kutokana na vitendo vya ujambazi ambayo vinausisha matumizi ya silaha zinazomilikiwa nje ya sheria

Rais Kikwete katika zaira yake wilayani Biharamuro mkoani Kagera amekemea vikali vitendo vya ujambazi hasa katika maeneo ya kanda ziwa na mikoa ya jirani nakuwate wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kizisalimisha.

Katika ziara hii Rais ameweka jiwe la Msingi la barabara ya Kigoma-Lusahunga Yenye Urefu Wa Kilometa Mia Moja Hamsini Na Nne. Barabara hii imejengwa kwa asilimia mia moja na serikali ya Tanzania.

Naye Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amezitaka Halmashauri nchini kutumia fedha za mfuko wa barabara kama zilivyopangwa na serikali.

Awali Rais KIKWETE alipokewa kwa shangwe zilizoambatana na ngoma za asili.
Next Post Previous Post
Bukobawadau