HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE YAVUNJWA KYERWA YAANZA RASMI • Uchaguzi wa Wenyeviti Wafanyika Kuwapata Wenyeviti Wapya • Mwenyekiti na Makamu Wake Wachukua Halmashauri Zote Mbili
Wananchi na Madiwani Waliokuwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Wakishuhudia Kuvunjwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Kuundwa Halmashauri mbili
Mhe. Massawe Akimkabidhi Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bw. George Mkindo Hati ya Kuanzishwa Rasmi Halmashauri Hiyo Wilayani Karagwe.
Bw. George Mkindo Mkurugenzi Mtendaji Kyerwa Akionyesha kwa Wananchi na Madiwani Hati ya Kuanzishwa Rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I Massawe Akilihubia Balaza la Madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
yaanza rasmi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I.
Massawe kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na kuundwa Halmashauri mbili
Karagwe na Kyerwa Julai 31, 2013.
Hatua hiyo ilitanguliwa na
uzinduzi rasmi wa wilaya 19 mpya nchini
ikiwemo Kyerwa uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete katika wilaya mpya ya
Kyerwa wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kagera Julai 27, 2013.
Kabla ya kuivunja Halmashauri ya
Wilaya ya Karagwe Mhe. Massawe
Aliwashukuru madiwani kwa kuendesha mchakato wa kuunda halmashauri mpya ya
Kyerwa kwa amani na utulivu na kusikilizana
ikiwemo kugawana mali na rasilimali za Wilaya mama ya Karagwe bila
malumbano.
Mhe. Massawe alisema kuundwa Halmashauri
mpya ni lengo la serikali kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi ili
kurahisha utoaji wa huduma hizo ambapo alisema mwaka 2005 Wilaya ya Karagwe
ilikuwa na shule 194 lakini kufikia mwaka 2013 zimejengwa shule na kufika 205.
Vile vile mwaka 2005 maji
yalikuwa yanapatikana Wilayani Karagwe kwa ujazo wa lita 125 lakini kufikia mwaka 2013 zinapatikana lita za ujazo 254 na
kuwahudumia wateja 445. Aidha, mwaka
2005 vilikuwepo Vyama vya Msingi 53 na SACCOS 14, kufikia mwaka 2013
Vyama vya Msingi 79 na SACCOS 79.
Mkuu wa Mkoa alisema hizo ni juhudi
za serikali katika kuhakikisha huduma
kwa wananchi zinaboreshwa na ndiyo maana serikali iliridhia kuanzishwa
kwa Wilaya mpya ya Kyerwa. Baada ya ufafanuzi huo Mkuu wa Mkoa alitamka rasmi
kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Aidha, baada ya kuivunja
Halmashauri ya Wilaya Karagwe alimkabidhi hati ya kuanzishwa Halmashauri ya
Wilaya ya Kyerwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bw. George Mkindo ambapo
ilipelekea kufanyika uchaguzi wa wenyeviti wa Halmashauri zote mbili siku ya
pili yake.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bw. Singsbert Kashuju alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya
Mpya ya Kyerwa na aliyekuwa makamu wake
Bw. Wales Mashanda alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Karagwe.
Hoja za Ukaguzi Katika Halmashauri
za Wilaya.
Katika hatua nyingine Mhe.
Massawe alihudhuria vikao maalum katika Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Kagera
na kujadili taarifa za hoja za ukaguzi za Mkuaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha ya
serikali ili kuhakikisha hoja hizo zinafungwa na fedha ya serikali inatumika
kama ilivyokusudiwa.
Katika majadiliano hayo kwenye
vikao maalum Mhe. Massawe alisistiza Mabaraza hayo ya Madiwani kuzisimamia
Halamashauri hasa watendaji kujibu hoja kwa wakati, Kupunguza utegemezi wa
Serikali Kuu na kubuni vyanzo vipya vya
mapato katika Halmashauri zao.
Pia kutumia fedha za miradi ya
maendeleo kwa wakati, Madiwani kutohusika katika wizi wa fedha za Halmashauri
za Wilaya na kutangaza maslahi binafsi pale wanapohusika katika kupata tenda za
miradi ya Halmashauri zao.
Aidha Mhe. Massawe alitoa siku
saba kwa kila Halmashauri ya Wilaya Mkurugenzi kuhakikisha watumishi wote
waliochukua masurufu bila kurejesha warejeshe ndani ya siku saba baada ya vikao
kwa kila halmashauri na wasiporejesha
wakatwe kwenye mishahara yao na apewe taarifa.
Ufuatao ni ukaguzi wa miaka
mitano kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008 mpaka 2011/2012 na Halmashauri za
wilaya za Mkoa wa Kagera zilipata hati zifuatazo: Missenyi hati safi miaka 5,
Biharamulo Hati safi miaka 5, Bukoba hati safi 4 na hati ya mashaka 1.
Bukoba Manispaa hati safi 4 na
hati ya mashaka 1, Muleba hati safi 4 hati ya mashaka 1, Karagwe hati safi 3
hati za mashaka 2, Ngara hati safi 3 hati za mashaka 2. Mkuu wa mkoa kujadili
hoza za ukaguzi katika Halmashauri za
Wilaya ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muunganoa wa Tanzania la April 29 2009.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013