Bukobawadau

KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA BAADA YA KIFO CHA MZEE JAMES BUKUMBI (BABA MZAZI WA ERIC SHIGONGO)

Padri Zenobius Mtewele akiongoza ibada ya kumbukumbu.

Eric Shigongo akiwa katika maombi.

Waumini wakifuatilia ibada.

Mke wa marehemu, Asteria Bukumbi akipewa kumunio.

Wanakwaya walioipamba ibada hiyo.

Waumini wa Roman Catholic wakikomunika wakati wa ibada hiyo.
Mzee Muhidini Gurumo (kulia) akipata chakula. Kushoto ni Juma Mbizo.

Mtoto wa marehemu, Masha Bukumbi (kushoto) akiteta jambo.

Waumini wakiendelea na ibada.

Waalikwa wakijiandaa kwenda kupata chakula.

Mmoja wa wahariri wa Global Publishers, Elvan Stambuli akiteta na padre aliyeendesha ibada hiyo.

Padri akifunga ibada kwa sala.

Shigongo akisalimiana na waalikwa.

Padri akiagana na Masha Bukumbi mara baada ya ibada kumalizika.

Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric James Shigongo na familia yake jana waliandaa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa baba yao mzazi, Mzee James Bukumbi nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar. Marehemu Mzee James Bukumbi alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Agosti 26, 2012 jijini Dar es Salaam. Katika kumbukumbu hiyo, kulikuwa na ibada ambapo watu mbalimbali walijumuika na familia ya Shigongo.
(PICHA NA HABARI: HARUNI SANCHAWA /GPL)

Next Post Previous Post
Bukobawadau