MCHAKATO WA MAENDELEO BUKOBA MAJIBU YANATAKIWA!
Ukweli wa mambo ni kwamba karibu kila sehemu ya maisha Bukoba “imesahauliwa” na Serikali yetu.
Usafiri ..
*Usafiri Wa Ndege ni aghali saana, haugusiki,
*Wa majini sasa ni hatari na wa kutisha na
* Wa barabara majambazi wametusubiri kututeka
Usalama… Uvamiaji wa wananchi wa Rutoro unasikitisha na kuna hatari inakuja mpakani.
Elimu duni … Karne ya 21 shule zetu hazina umeme, hazina maji, hazina computer, madawati, walimu wa kutosha
Magonjwa ya mazao (Mnyauko na mengine) hayashughulikiwi.
Miradi ya maendeleo ..Bukoba inawekwa pembeni.Rubafu? Umeme, MCC I na MCC II Bukoba imetengwa.
Huduma za Afya..Mbaya sana na madawa mpaka uonge kwenye dirisha hospitali ili upate dawa.
Nitazungumzia mawili tu nisiwachoshe. (usafiri na Usalama)
Usafiri:
Meli ya Victoria ilianza kufanya kazi kwenye karne ya 19 na ikaletwa Rwelu mnamo 1932 ikiwa imeshatumika.. Sasa dalili za kutokomeza ndugu zetu zimeshajionyesha na taadhari zimeshatolewa ila hazitiliwi maanani. Kabla MV Bukoba haijazama 26/05/1996, taadhari zilitolewa kama zinazotolewa sasa za Victoria lakini zilifungiwa macho.
Ilipozama serikali yetu ilituma askari mmoja na “cutting torch” aidha makusudi au bila ufahamu wa “bouyance” akatoboa tundu na zaidi ya watu 1,000 wakatokomea wengine wakipiga simu kuomba kusaidiwa.
Victoria muda wake umekwisha na Serikali isisubiri mpaka itokomeze maelfu ya ndugu na watoto wetu. Nd. Kikwete aliahidi Meli mpya mwaka 2010 kwamba itakuwepo by December 2011, lakini mpaka sasa hamna dalili zozote. We need answers.
Omukajunguti:
Tukiwa na uwanja wa kimataifa safari Mwz – BKB itakuwa kadilia + sh 60,000 kwa FAST JET na chini ya masaa 2.
Uwanja wa ndege Bukoba (400m or so) haukupigwa rami na wa matope kwa zaidi ya miaka 50. Kisingizio kipi serikali inatupa kwa hili?
Kama kweli Raisi Kikwete alimaanisha ukweli kwamba Uwanja wa mataifa unajengwa, tunaomba wabunge watupe tarehe ambapo huu mradi utaanza na unategemea kumalizika lini? Hapo ndipo tutaweza kujua kama kweli Nd. Kikwete amekuja na matumaini na sio kwa campaign za kura za CCM.
Usalama:
kuna sehemu nilisoma baadhi ya repoti nzuri toka web link kuhusu hali halisi ya mpakani na Rwanda… inasikitisha sana.
Wananchi wa Rutoro mpakani na Rwanda wapo hatarini na wanaishi kwa woga. Wale ambao hawafahamu uwezo wa hawa majirani zetu, wasikilize wanavyowasumbua na kuwaua wenzetu DRC. Hata Jeshi la Joseph Kabila limeshindwa kuwaondoa. Abanyarwanda wanatumia mabavu.
Usipoziba ufa utajenga ukuta usiojengeka kama DRC.
Serikali yetu inabidi tena haraka kuingilia kati mapema na kuimalisha huu mpaka kabla hali ya DRC haijatuingilia.
Jeshi la wananchi linalipwa vizuri sana na linapewa bidhaa za bei rahisi kila siku na marupurupu mengi (subsdised commodities); waje wajenge vituo vya jeshi huko palipo na matata; na sio Dar es Salaam au mijini. Jeshi letu lisiwe jeshi la kulinda masilahi ya mshika hatamu, bali liwe jeshi la wananci na kulinda wananchi. Huko mpakani kuna hatari na kuziba ufa iwe priority na tena haraka. Barugeyo baije bajune eiyanga.
KUMALIZIA.
Ningeomba Wahusika Mkoa na Wabunge wetu wote watutayarishie jumwisho (summary)wa yote kuhusu ziara ya Raisi, ikieleza ahadi na miradi yote iliyozungumziwa wakati wa ziara na siku gani zitatekelezwa. Hasa Omukajunguti na Meli mpya.
Tumetengwa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi ch…, tumenyimwa haki kiasi.., tumedharauliwa…tumepuuzwa kias.., tumepigwa vita mda mrefu na kupewa ahadi za udanganyifu.
Sasa tunataka ukweli na tunautaka jana na sio leo.
Bila usafiri nafuu, maendeleo Bukoba yatakuwa magumu. Hatutaki kuchezewa tena.
Waitu naeleza mulanganyila byalaiya muno
Imetolewa na Mdau