Ngoma Africa Band kuvaana na washabiki International African Festival Tubingen 2013 Siku ya Ijumaa 9 na Jumamosi 10 .08.2013 Tubingen,Germany
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" a.k.a FFU ughaibuni,inatarajiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya International African Festival Tubingen 2013, huko Ujerumani.
Bendi hiyo yenye washabiki lukuki kila kona duniani imejikuta kwa mara nyingine tena kupambambanishwa na washabiki sugu katika maonyesho hayo makubwa,
Kutokana na matakwa wa wapenzi na washabiki, bendi hiyo imepewa siku mbili
kutumbuiza juu ya jukwaa kuanzia siku ya ijumaa 9 na Jumamosi 10.08.2013.
Watayarishaji wa onyesho hilo wameamua kuipa siku mbili bendi hiyo kuwaridhisha Wapenzi na washabiki wa bendi hiyo.
tuwasikilize FFU ughaibuni katika kambi yao at www.ngoma-africa.com au htt p://www.ngoma-africa.com