Wema Sepetu ajaza umati wa watu mahakamani, ni katika kesi yake inayomkabili
Mwanadada Wema sepetu amegeuka kivutio kikubwa katika eneo la mahakama ya Kawe Jijini Dar es Salaam katika kesi yake inayomkabili ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu GPL wameripoti.
Habari hiyo inasema Katika mahakama hiyo watu walifurika kwa lengo la kutaka kumuona Wema aliyepandishwa mbele ya Hakimu, Bernice Ikanda kusomewa mashtaka ya kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Goodluck.
Wema aliyekuja mahakamani hapo na msafara wa wafanyakazi na wapambe wake wakiwa na gari tatu tofauti aina ya Audi Q 7, Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa yamejaza wapambe wake.
Kesi hiyo imehairishwa tena mpaka agosti ishirini mwaka huu baada ya upande wa mashitaka kutakiwa kuleta mashahidi wengine Zaidi.