CHECK KIMBEMBE HIKI MWANAMKE MWENDAWAZIMU AKUTWA NA MAITI YA MTOTO MGONGONI!!!!
Ni tukio la hivi karibuni lilitokea Mitaa ya Migeyo ndani ya manispaa ya Mji wa Bukoba.
Pichani ni mkusanyiko wa watu na Polisi wakiwa eneo la tukio baada ya wananchi kutoa taarifa juu ya mwanamke mmoja ambaye ni kichaa kwa kujulikana, aliyekua akitembea na maiti ya mtoto wake mgongoni pasipo kujua,Kwa uzoefu wa baadhi ya wadau kwa kutumia macho yao tu ile muhaya anasema 'ELISHO ELYOBUKULU' au 'OKWONAMBONA' wanasema mtoto huyo inavyo onekana amefariki ndani ya siku mbili zilizopitabila .
Mkusanyiko wa mashuhuda katika kimbembe hiki cha kusikitisha.
Muonekano wa maiti ya mtoto ikiwa imelazwa kwa chini mara baada ya kutolewa Mgongoni mwa mama huyo anayesifika kama chapombe kutokana na ulevi uliopitiliza pamoja na uwenda wazimu wake.
Mashuhuda wakiendeleza 'kaulule',wakiongea na bukobawada mashuhuda wa mwanzo wanasema ,walishangaa kuona mtoto aliyebebwa na mwanamke huyo shingo imepinda,hivyo wakachukua jukumu la kutaka kumsaidia ili kumuweka mtoto vizuri,na hapo ndipo ilipogundulika mtoto huyo amefariki.
Huyu ndiye Mwanamke mwendawazimu mama mzazi wa marehemu akiwa ajielewi na kutojua nini kinaendelea baada ya kukutwa kabeba maiti ya mtoto kama abebavyo mtoto mzima mgongoni
Hadi tunaingia mtamboni Polisi tayari wameuchukuana mwili huo katika hospital kuu ya Mkoa kwa ajili ya uchunguzi.
Hakika si Wote wanaozaa na wenye uwezo wakuzaa wanasifa ya kuwa mama!!