Filikunjombe ‘amwaga’ pikipiki
Ludewa. Mbunge wa Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe, ametoa msaada wa vifaa mbalimbali na pikipiki 34 kwa madiwani wote 34 wa Kata za Halmashauri ya Ludewa, kwa lengo kuwarahisisisha usafiri katika kutoa huduma kwa jamii.
Pikipiki hizo zilikabidhiwa hivi karibuni na Katibu wa Mbunge huyo, Stanley Golwele.
Kwa mujibu wa katibu huyo, vyombo hivyo vimegawiwa bila kujali itikadi za vyama vya siasa.
Pia amekabidhi mipira mitano kwa kila diwani ili itumike katika kuhamasisha vijana kupenda michezo na kuepuka kujihusisha na ngono.
Gowele alisema hatua hiyo ni mbunge huyo kutumiza ahadi aliyotoa miaka miwili iliyopita ya kuwasaidia madiwani kupata usafiri wa pikipiki.
CHANZO;MWANANCHI