OPERESHENI KIMBUNGA YAANZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA WAHAMIAJI HARAMU, MAJAMBAZI NA SIRAHA VYAFICHULIWA
Mhe. Massawe na Kamanda Simon Sirro Msaidizi wa Kamanda wa Operesheni Kimbunga Wakiongea na Waandishi wa Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Katikati Akisistiza Jambo kwa Waandishi wa Habari
Hivi ni Vyombo vya Habari Kwa ajili ya Kuwajulisha Wananchi nini Kinaendelea na Wazee wa Kazi Wakiwa Kazini
Waandishi wa Habari Wakiwa Kazini Wakati wa Kupata Habari Juu ya Operesheni Kimbunga
Huu ni Mfano wa Picha ya Baadhi ya Aina za Siraha Zinazotumiwa na Majambazi Kuteka Wananchi na Mali zao Nchini
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Katikati Akisistiza Jambo kwa Waandishi wa Habari
Hivi ni Vyombo vya Habari Kwa ajili ya Kuwajulisha Wananchi nini Kinaendelea na Wazee wa Kazi Wakiwa Kazini
Waandishi wa Habari Wakiwa Kazini Wakati wa Kupata Habari Juu ya Operesheni Kimbunga
Huu ni Mfano wa Picha ya Baadhi ya Aina za Siraha Zinazotumiwa na Majambazi Kuteka Wananchi na Mali zao Nchini
Operesheni kimbunga ya kuwasaka
wahamiaji haramu, majambazi na siraha za kivita imeanza kuonyesha ufanisi
mkubwa baada ya siku mbili kuanza tayari wahamiaji haramu 1850 wametiwa
mbaloni, siraha 7 zimekamatwa, na ng’ombe 1765 zimekamatwa katika mapori ya akiba.
Taarifa hiyo ilitolewa katika
mkutano wa waandishi wa habari Jumapili tarehe 8/09/2013 na Kamanda Simon Sirro
Mkuu wa Operesheni za Polisi nchini ambaye ni msaidizi wa Kamanda wa
Operesheni Kimbunga ya kuwasaka wahamiaji haramu, siraha na
majambazi katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Kamanda Sirro alisema operesheni
hiyo ilianza tarehe 6/09/2013 na kufikia tarehe 8/09/2013 katika Mkoa wa Kagera
wahamiaji haramu waliokamatwa ni 750, bunduki (magobole) 2, na ng’ombe 1323. Mkoa
wa Kigoma wahamiaji haramu 855, Bunduki 2, na ng’ombe 200.
Pia katika mkoa wa Geita
wameishakamatwa wahamiaji haramu 246, Bunduki magobole 3, ng’ombe 240 sare moja
ya Jeshi la wananchi Tanzania. Ng’ombe walikamatwa katika mapori ya akiba ya
Moyovosi Kigoma, Burigi Kagera (Karagwe na Kyerwa) na maeneo mbalimbali ya mkoa
wa Geita.
Katika hatua niyingine Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian Massawe alisema tarehe 26/07/2013 baada ya Rais Kikwete
kuagiza wahamiaji haramu kuondoka kwa
hiari na majambazi kujisalimisha na siraha zao kabla ya operesheni kimbunga, walioondika
kwa hiari ni 11,601.
Aidha siraha zilizosalimishwa ni
65 (SMG 3, Shortgun 10, Magobole 52) na siraha hizo nyingi zilipatikana katika
wilaya ya Biharamulo. Pia Mhe. Massawe alisema ilitarajiwa waondoke wahamiaji
haramu 52,000 mpaka 53,000 lakini mpaka operesheni inaanza waliondoka 11,601 na
wengi kubaki nchini.
Angalizo, Kamanda Sirro alitoa angalizo na kuonya wanananchi
watakaogundulika kuwaficha wahamiaji haramu kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria, pia
jambazi yeyote atakayetaka kutumia siraha kujihamia atakiona cha moto kutoka
vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoondesha operesheni hiyo.
Pia Kamanda Sirro aliwahakikishia
wananchi kuwa operesheni kimbunga hiyo itazingatia haki za binadamu na hakuna
mtu yeyote atakayeonewa wala kunyanyaswa au kunyanganywa mali zake kwa nguvu.
Imeandikwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013