WANANCHI WA TARAFA YA KAMACHUMU WAAMUA KUWEKEZA KATIKA ELIMU
Wananchi wa Tarafa Kamachumu wameamua kutumia rasilimali zao kuongeza kasi ya kuchangia Elimu katika Tarafa yao na Mkoa kwa ujumla kwa kuamua kujenga shule ya sekondari nyingine Tarafani humo.
Wazo hili lilianzishwa kwa mara ya kwanza wanakijiji wa Kijiji cha Bushagara, Kata Kamachumu siku ya harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Kamachumu (A’hamugongo). Katika harambee hiyo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Kagera wa wakati huo kanali Mstaafu Enos Mfuuru, wanakijiji wa kijiji cha Bushagara walimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa, watoto wao wanatembea umbali mrefu kutoka Kijijini kwao kufika kwenye shule hii ambayo ni ya kutwa, hata hivyo shule za sekondari zilizopo, hazikidhi hitaji la elimu kwani kata ina shule za msingi nyingi hivyo wanafunzi wengine hubaki bila kuchaguliwa kutokana na kukosa nafasi kwenye shule za sokondari zilizopo.
Mkuu wa Mkoa aliunga mkono wazo la wanakijiji hao mara moja na kuwaimiza waanze mipango ya ujenzi kwa kufuata taratibu za serikali. Mipango ilianza, Kamati ziliundwa na michango ikaanza kijijini na Wilaya ikatoa kibali cha Ujenzi. Aidha, baadaye ilionekana Kijiji peke yake hakiwezi kumaliza kazi hii, ndipo Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ikaamua shule hii iwe ya Kata.
Hadi sasa hivi, msingi wa vyumba vya madarasa manne umemalizika, jamvi limemwagwa na wakati wowote ujenzi wa kuta utaanza. Shule hii inajengwa katika maeneo yaliyo karibu na shule ya msingi Ndolage na itajulikana kwa jina la “Shule ya Sekondari Ndolage”.
Kamati anzilishi inayosimamia ujenzi ina wajumbe wafuatao:
1. Dr. Calixte Twagilayezu - Mwenyekiti wa Kamati
2. Dr. Emmanuel Rwabukambwe – Mtunza Hazina wa mradi
3. Bi. Dinah Kaimukilwa - Katibu wa kamati
4. Prof. Wilson Niwagila – Mjumbe
5. Mr. Yusto P. Muchuruza – Mhamasishaji na Mawasiliano
6. Mr. Sempholian Nkokelwa – Mwenyekiti wa Kijiji Bushagara
7. Rev. Brighton Kahigi – Mjumbe
8. Mwinj. Joshwa Ndyakukama - Mjumbe
9. Bi. Grace Batenga – Mjumbe
10. Bi. Nesta Lutosha – Mjubme
11. Bi. Alferdina Balige – Mjumbe
12. Afisa Mtendaji wa Kata - Mjumbe
13. Mratibe Eimu Kata - Mumbe
Aidha, Kamati inamkumbuka na kumuenzi Marehemu Sheikh Jafari Bwanika ambaye alikuwa kati ya waanzilishi lakini Mungu alimpenda zaidi mwanzoni mwa mwaka huu.
Aidha, tunawashukuru wote ambao tayari wameishatoa michango ya hali na mali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Mheshimiwa Charles Mwijage ambaye ametoa Tshs. 1,000,000/=, Matofali 40,000 na trip mbili za kokoto. Wengine ni Bw. Gozibert Protazi Aliyetoa 600,000/= ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kujenga chumba cha darasa, Bw. Yusto Muchuruza aliyetoa 300,000/= na vitu vingine in kind, CCM Kata Kamachumu (Mifuko 50 ya saruji) CCM Tawi Kamachumu (Mifuko 10 ya saruji), Bw. Festo Rweyemamu (trip moja ya mchanga), Prof. Wilson Niwagila (200,000/=), Dr. Twagilayezu (200,000/=), Bw. James Niwagila ambaye amechora ramani za majengo bure (thamamni ya 3,000,000), Bnonofsce Katanyebile (50,000/=), Bw. Paulin Rwezaula (50,000/=), Mzee Semohlian aliyetoa mchango wake kwa vitu (in kind) na wengine wengi ambao hatukuwataja. Wote wanastahili shukrani za wanatarafa Kamachumu.
Kwa kutambua kuwa wewe ni mdau wa Elimu na mpenda maendeleo, Kamati ya Ujenzi inawaomba wote wenye mapenzi mema, wadau wa elimu na wapenda maendeleo kuunga mkono jitihada hizi kwa kuchangia hali na mali ili kufanikisha azma hii.
Aidha, kamati inawaomba wote kututafutia wafadhili au marafiki wengine wa kutuunga mkono kufanikisha mradi huu.
Gharama zote za mradi huu zimekisiwa kuwa Tshs. 723,429,454.00 ambazo zinategemewa kupatikana katika awamu nne za mwaka mmoja mmoja (2013-2016). Bajeti ya mwaka huu 2013 ni Tshs. 106,570,860/=.
Tumehaidiwa kupewa wanafunzi 2014, tumehaidiwa kupewa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwezi January 2014 endapo tutakamilisha mahitaji yanayotakiwa (vyumba vinne vya madarasa, vyoo matundu 8, choo ya walimu matundu 4 na ofisi ya walimu).
Tunaomba michango yote itumwe kwenye akaunti ya Benki ya CRDB Na: 0152215530400; SWIFT CODE: CRDBCORUTZTZ au wasiliana na Mwenyekiti wa Mradi huu Dr. Twagilayezu kwa namba ya simu 255713455240, E-mail: ndola.seko@gmail.com, au Mwenyekiti wa Kijiji Bushagara
Bw. Sempholian Nkokelwa 0754421233.
Tunatanguliza shukrani za jamii ya Tarafa Kamachumu kwa wote wanaotuunga mkono ndani na nje ya Tarafa.
Imetolewa na:Muchuruza, Y.P.
MUHAMASISHAJI