Bukobawadau

WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole, baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali.
Next Post Previous Post
Bukobawadau