Family Day Bonanza la Skylight Band ndani ya kiota cha Escape One palikuwa hapatoshi Jumapili hii
Nguvu kazi ya Skylight Band ikiongozwa na Sam Mapenzi kutoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo ndani ya kiota cha Escape One kwenye Family Day Bonanza kila siku ya Jumapili kuanzia Saa 10 jioni kwenye hewa safi na upepo mwanana wa Baharini.
Superstar Mboni Masimba na rafiki yake nao walikuwepo kwenye kiota cha Escape One kupata burudani ya Skylight Band.
Mdogo mdogo wadau walianza kujisogeza pande zile.
Eneo kubwa la kujinafasi kwenye kiota cha Escape One ukiamua kukaa gorofani haya wewe tu na chaguo lako.
Aneth Kushaba AK 47 akifanya yake Escape One huku akiwa na muonekano mpya wa nywele ukizipenda ongea nae upendeze kama yeye alivyong'ara.
Warembo walikuwepo wakumwaga kwa raha zao wakijinafasa na Skylight Band kiota cha Escape One Jumapili hii.
Mary Lucos akifanya yake jukwaani ndani ya kiota cha Escape One.
Bwana Felix (aliyebeba mtoto) akiwa na familia yake kwenye kiota cha Escape One alipokuja kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na Skylight Band.
Birthday boy Felix akilishwa cake na mkewe alipokuwa akiimbia wimbo wa Happy Birthday na Skylight Band.
Mke wa Felix akaona hata ale peke yake tu...lazima ni muonjee birthday boy....
Familia ya Felix ikonyesha furaha isiyona kifani.
Birthday Boy Felix na mkewe wakiwapungia waimbaji wa Skylight Band( hawapo pichani)kuwashukuru baada ya kumwimbia na kumtakia Heri ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Hapana chezea Skylight Band wewe.....utapata burudani za vijana kwa wazee njoo Jumapili hii wewe na familia yake kwenye Family Day Bonanza la Skylight Band.
Mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka kwenye kiota cha Escape One Jumalii hii kwenye Family Day Bonanza.
Hapo sasa bwana weweeeeeeee....ni balaaaaa!
Alois Ngonyani, Mheshimiwa Bunda na mdau Emma wakisakata Sebene huku Sony Masamba akitumbuiza.
Mduara haukukosekana pia nao ulihusika...wa mbele aende mbele na wa nyuma arudi nyuma...
Mwanadada Happy yupo kwa ajili ya kutoa huduma ya Ice Cream za kila aina kwa mtoto wako kwenye Family Day Bonanza la Skylight Band ndani ya Escape One.
Ma-producer wakali wa mjini nao walikuwepo kuipa shavu Skylight Band..... Kutoka kulia ni Producer Dunga (Mandugu Digital), P-Funk (Bongo records), Lamar pamoja na Lubea wa Skylight Band wakipata Ukodak.
MC Mkali wa town Adam Mchovu akishow love na Lubea wa Skylight Band.
Hot and cute babes were also there.
Mtangazaji wa Channel Ten na Magic Fm Salma Msangi naye alikuwepo ndani ya kiota cha Escape One.
Camera yetu inazidi kupata mashabiki wa Ukodak.......Mwanadada mrembo shabiki wa Skylight Band akipata Ukodak.
Marafiki walioshibana wakipata Ukodak na tabasamu bashasha kwenye nyuso zao.
Dj Bike wa Radio One Stereo naye alikuwepo.
Wakali wa town..Kutoka kushoto ni Julio Batalia, Chege Chigunda, DJ Bike, Madee pamoja na P-Funk Majani wakishow love ndani ya kiota cha Escape One na burudani ya Skylight Band Jumapili hii.
Mashabiki wa ukweeeh wa Skylight Band wakiapata Ukodak.
Mwanadada Jacky akishow love na marafiki zake ndani Escape One wakati wa burudani ya Familiy Day Bonanza la Skylight Band Jumapili hii.
Wadada wa warembo wakipata Ukodak.
Mboni Masimba na shosti wake Masha wakishow love na Ukodak.
Salma Msangi na mashosti zake ndani ya Escape One na Family Day Bonanza la Skylight Band Jumapili hii...mwambie yule na wale wasikose Jumapili ijayo.
Joniko Flower wa Skylight Band na mashabiki wake.