KAPOTIVE STAR SINGERS-BUKOBA KUWASHA MOTO GOLD CREST HOTEL-MWANZA MWEMA JUMAPILI HII TAR.06/10/13.
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE
Star Singers- Bukoba kitafanya uzinduzi wa album yake nzuri sana ya Yesu ni Mwema, na utambulisho wa album
nyingine kama “Nakushukuru Mungu”, “Zawadi ya Krismass n.k siku ya Jumapili tar. 06/10/2013 katika ukumbi wa Gold
Crest hotel- Mwanza.
Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Samuel
Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na mgeni maalum atakuwa Baba
Akofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba ambae pia ni
mlezi wa kikundi hiki.
MC katika uzinduzi huo atakuwa Bw. Bernard Mukasa, mtunzi
ahiri wa nyimbo za Dini, na watasindikizwa na mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili
Dada Christina Shusho, kwaya ya Mt.
Benedicto parokia ya Bugando, na kwaya ya vijana ya AIC-Bwiru.
Kiingilio kitakuwa 15,000 kwa mtu mmoja (single size ticket)
na 50,000 kwa watu 4 (Family size ticket).
KAPOTIVE Star Singers_Bukoba wamejizolea umaarufu katika
uimbaji mahiri, na maonesho yao makubwa ambayo yamefanyika Bukoba na
Dar-es-Salaam yaliwavutia wengi.
Watu wa Mwanza msikose burudani ya aina yake siku ya Jumapili
tar. 06/10/13 katika ukumbi wa Gold Crest-Hotel, katikati ya jiji la Mwanza.
Karibu tuwaunge mkono vijana wetu.