KUTANA NA MWANAHARAKATI WA KUGOMBEA HAKI ZA MTOTO WA KIKE KUTOKA MAREKANI ALIYETUA DAR JANA
Anaitwa Zuriel Oduwole, msichana mdogo wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, yupo jijini Dar es salaam hivi tunavyoongea akiwa na wazazi wake na wadogo zake watatu, katika harakati zake za kupigia chapuo umuhimu wa kumuendeleza mtoto wa kike katika Afrika.
Tayari Zuriel ameshafanya mahojiano na Marais wanane (akiwemo Rais Kikwete) pamoja na Waziri Mkuu wanne wa Afrika, pamoja na mfanyabiashara tajiri kuliko wote Afrika Bw. Dangote, hali kadhalika nyota wa tennis duniani toka Marekani, Venus na Serena Williams.
Zuriel, ambaye ni mtengezea filamu, mwanahabari na mwanaharakati wa maslahi ya wasishana wadogo, yuko nchini akitokea Malawi ambako kama ilivyokuwa hako, hapa nchini, hususan jijini Dar es salaam, atafanya mihadhara katika shule kadhaa ya kuhamasisha wasichana wadogo wajiamini na kusaidia katika kuzungusha gurumu la maendeleo huku wakipiga vita unyanyapaa dhidi yao. Mwezi Agosti mwaka huu Zureil aliweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote waliopata kuhojiwa na jarida maarufu la watu maarufu na matajiri duniani la Forbes. VHapideo ya hapo chini kabisa ni moja ya vipindi alivyoandaa:
Zureil akimhoji Rais wa Liberia Mhe Mama Ellen Johnson Sirleaf
Zureil akimhoji Rais wa Nigerai Mhe Goodluck Jonathan
Zureil akimhoji Mhe Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Zureil akimhoji Rais wa Cape Verde Mhe Jorge Carlos Fonseca |
Zuriel akiongea na Rais Jakaya Kikwete |
Zuriel akimhoji Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Salva Kiir Mayardit |