MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA SHULE YA SEKONDARI KISHOJU
BUKOBAWADAU
9 Oct, 2013
Jumuiya ya Shule ya Sekondari Kishoju pamoja na bodi ya shule wanayofuraha kukukaribisha wewe kwenye maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa Kishoju sekondari 1978. Sherehe kubwa hii itatanguliwa na mahafari ya kidato cha Nne pia kutakuwepo na harambee ya kusaidia ukarabati wa shule itakayofanyika tarehe 24 October 2013 shuleni Kishoju kuanzia saa nne asubuhi. Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe.
Kipaumbele ni kwa hisani ya wanafunzi waliosomea Kishoju tangu kuanza kwake pamoja na wadau wote wa elimu na maendeleo Kagera, viongozi wote wa Mkoa wa Kagera- Safari hii sio kwa hisani ya Wamarekani.
Mimi William Oswald Rutta ( Willy Kiroyera) pia ni zao la Kishoju A level ya 1993 nimechanguliwa na kamati ya Maadalizi kuhamasisha wadau wote walioko nje ya Wilaya ya Muleba na nje ya Mkoa kupitia mitandao ya kijamii , radio na tevevision.
Unaombwa kufanikisha kwa kuwepo siku hiyo 24/10/2013 au kwa kuchangia moja kwa moja kwenye Acount ya Shule hapa chini
Jina la account: MULEBA DISTRICT COUNCIL KISHOJU SECONDARY SCHOOL
Account Number: 32001200049
Bank Name: NMB MULEBA BRANCH
Harambee hii itakuwa ya aina yake maana ukiweza kwa kukarabati darasa au bweni basi jina lako litaandikwa kwenye bweni au darasa tajwa, Pia unaweza ukawezesha kwa vifaa vya ujezi, Vitabu vya Advanced level (History Geography, Language), Vifaa vya Michezo, jiko liko khali mbaya pia. unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mkuu wa Shule Bi Witness Amos namba za simu +255 754 355 961 ili mchango wako uwezwe kusomwa na kutangazwa siku ya Harambee shuleni Kis hoju kwa wale ambao hawataweza kufika.
ona sehemu ya chakula
Unaombwa pia kutuma majina ya wanafunzi unawakumbuka waliosome kishoju kwa Bw Willy Kiroyera 0756 823 250 au kwa email- williamrutta@gmail.com
Waitu mbakasinge
William Oswald Rutta
Co ordinator wa kuhamasisha
Wadau wakikagua mazingira ya shule.Vyombo vya chakula.
Mdau Geofrey mmoja wa wanafunzi aliyepitia shulieni hapa.
Mdau Hassani Milanga pichani
Muonekano wa hali ya jikoni
Muonekano wa mabweni ya shule ya sekondari Kishoju
Kiroyera Tours
www.kiroyeratours.com
www.kagera.org
www.budap.org
http://www.facebook.com/pages/ Kiroyera-Tours-and-Consulting/ 171058592931255
http://www.twitter.com/ kiroyeratours
http://www.youtube.com/user/ kiroyeratours
P.O. BOX 485
BUKOBA, KAGERA, TANZANIA
Tel: +255 28 2220203
Mobile: +255-784-568276
FAX: +255 28-2220009
Member of Tanzania Association of Tour Operator (TATO)
African Safari around Lake Victoria, Tour Operators, Travel Itinerary &
Booking Agents and Management Consultants
Cultural tours in Bukoba, Rubondo Island, Kigoma lake Tanganyika
Chimpanzees, Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro,
Rafting on the Nile, Gorillas in Uganda and Zanzibar Island
BUKOBAWADAU
Bukoba Wadau ni mtandao unao toa habari na matukio yanayo tokea katika mji wa bukoba pamoja na mkoa wa kagera kwa ujumla.
Email:bukobawadau@gmail.com | Phone :Mc baraka:0784 505045, 0754 505043
Instagram @bukobawadau | Facebook @bukobawadau