Bukobawadau

"Maji ya moto yaliyochemka yanaganda (kuwa barafu ) haraka zaidi kabla ya maji baridi” (Warmer water can freeze faster than colder water).

Ni ugunduzi wa kisayansi wa mtanzania usiotajwa kwenye vitabu, shule wala vyuo vyetu hapa Tanzania, lakini ni gumzo kwa mataifa ya nje na unaowaumiza vichwa wana sayansi wa kimagharibi na ki-asia!

Ugunduzi huu wa kisayansi unaeoelezea sifa ya kipekee ya maji, ulifanywa na mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Magamba, Lushoto, mwaka 1963, Erasto Mpemba! Ndipo sifa hiyo ya maji (physical phenomenon) ikaitwa kwa jina lake” The Mpemba effect”

Inasemwa “Science is all about exploring and discovering” (Sayansi ni kuchunguza na kugundua), na ili uweze kufanya uchunguzi na ugunduzi ni lazima uwe na tabia ya udadisi (curiosity). Wengi tunakutana na vitu visivyo vya kawaida wakati tunafanya shughuli zetu za kila siku, kama kupika, kufuwa n.k, lakini tunaishia kusema ndivyo ilivyo au Mungu kapanga hivyo. Lakini hata wale walioko mashuleni, vyuoni, au kwenye vituo vya utafiti, wakati wanapofanya tafiti zao hawashangazwi, wala kuvutiwa na “observations/phenomena” ngeni zinazojotokeza katika tafiti zao, hii ni kwa sababu majibu ya tafiti nyingi hulazimishwa yakidhi “hypothesis/theory” ya tafiti hizo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau