CKECK MATUKIO YA BONANZA LA TBL LILILOFANYIKA UWANJANI KAITABA NA BADAE SHANGWE KUENDELEA FUKWENI KIROYERA
Ni tukio la bonanza la Bukoba Veterani chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya TBL,pichani ni wachezaji wa timu ya bukoba Veterani wakipasha kabla ya mechi kuanza,Bonanza ilo uanzia kwa mechi ya wenyewe kwa wenyewe kwa timu mbili yaani Kahawa Fc na Banana Fc ambapo mshindi alikuwa Kahawa Fc na kuibuka na ushindi wa goli 2-1
Wachezaji wa timu ya Bukoba Veteran
Wachezaji wa timu ya Bukoba Veteran
Baada ya hapo ulitolewa muongozo na mwenyekiti Ernest Nyambo na wanachama na rafiki zao wote wakaamia viwanja vya beach Kiloyera kwa misosi na burudani zaidi
Bonanza likiendelea Wakiwa pembezoni mwa ziwa Victoria kiwanja maarufu kama Kiroyera Beach ,wadau kwa pamoja walipata vinywaji toka TBL na Msosi kabambe kutoka kwa Dada Hawa Hassan mmiliki wa mghahawa wa HHH
Kazi ilianza kutafuta bingwa wa mchezo wa drafti ,Mshindi alikuwa kaka moja kutoka Tarime mkoani mara aliyezuka tu kama msg na kuja kuwagaragaza bila huruma wana bukoba wote na kujinyakulia kitita cha sh.100000 laki moja na kwenda zake
Kazi ilianza kutafuta bingwa wa mchezo wa drafti ,Mshindi alikuwa kaka moja kutoka Tarime mkoani mara aliyezuka tu kama msg na kuja kuwagaragaza bila huruma wana bukoba wote na kujinyakulia kitita cha sh.100000 laki moja na kwenda zake
Mchakato mzima wa kupata msosi ukiendelea
Mchezaji Salum Big akionyesha uwezo wake wa kurap
Ndg Optaty Henry
Papaa Moses Mnyama.
Mwenyekiti Ernest Nyambo akitoa maelezo juu ya safari yao ya Arusha tarehe 11 wamealikwa na veteran wenzao wa huko wanaitwa KITAMBINOMA,hapo kaka mkuu akiwahimiza wadau kujumuika pamoja pia aliwajulisha wana Bukoba wote kuwa mdau Samwel Rugemalila wa Arusha amewaandalia wana Bk Veteran mapokezi mazito na maisha bora wakiwa mkoani Arusha
Mdau Lyimo na Mdau Sudi wakifuatilia jambo kwa umakini
Baada ya mashindano ya kucheza draft na kumtafuta mkali wa ku rap ,yakafuata mashindano ya kucheza muziki mchanganyiko kama inavyo onekana katika picha.
Kisanolo
BUKOBAWADAU BLOG TUNAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUWAOMBA SAMAHANI NA KUWATAHADHALISHA WASOMAJI WETU KUWA WATU WASIOJULIKANA WAMEWEZA KUHACK ACCOUNT YA PAGE YETU KUPITIA FACEBOOK NA HIVYO WANAITUMIA NDIVYO SIVYO KWA KUWAPOTOSHA WATU ,ANGALIZO NI KWAMBA HABARI ILIYOPO INAYODAI KUNA FOUNDATION YA MIKOPO ISIYO NA RIBA SIO SAHIHI KABISA NI MATAPELI WAKUBWA NA MPAKA SASA BADO IPO MIKONONI MWAO,TUMETOA MATANGAZO KUPITIA RADIO MBALIMBALI NA HAPA NI SEHEMU YA MUENDELEZO.
POLE SANA WALE WALIOINGIZWA
TUTAENDELEA KUPATIKANA KUPITIA BLOG YETU http:// bukobawadau.blogspot.com/ ,KUPITIA TWITTER(@Bukobawadau)na account binafsi za facebook ,tumblr na Instagram
Pia bukoba veteran ilitoa changamoto kwa kutafuta nani mkali wa kucheza wimbo wa my number one wa Diamond Platinum na binti mdogo wa miaka 13 aliyetambulika kwa aka Wema Sepetu akaibuka mshindi na kujinyakulia zawadi ya kwanza.
Mchuano wa nani mkali wa Draft.
Hakika ni bonge la shangwe.
Mdau Gilbart George
Timu nzima ya Bukobawadau Blog tunatoa pongezi sana kwa juhudi za bukoba veteran kuiweka bukoba kwenye ramani kama wafanyavyo mikoa mingine,tusikalie tu majungu badala ya kudumisha upendo furaha na kuchapa kazi pia tunawatia moyo ndg zetu wa Kagera wanaoishi Arusha juu ya kuwapokea jamaa zetu na kuwazungusha kwenye viunga vya jiji la A town, big up sana Mdau Samwel Rugemalila wa Victoria Expedition.