MH. JANUARY MAKAMBA AIPA SHAVU SKYLIGHT BAND
Kikosi kazi cha Skylight Band kikitoa burudani Juma lililopita kwa mashabiki wa Skylight Band akiwemo Mh. January Makamba aliyetembelea kiota cha Thai Village ku-refresh mind na burudani ya Band hiyo.Pichani kutoka kushoto ni Mary Luco, Joniko Flower, Digna pamoja na Sony Masamba.
Hebu cheki watasha walivyopagawa na burudani ya Skylight Band mpaka wakaamua kuchukua picha za kumbukumbu....Hapana Chezea Skylight Band.
Aneth Kushaba AK47 akionyesha machojo yake kwa mashabiki.
Mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka taratibu kwa kujinafasi.
Mary Lucos sambamba na Digna wakifanya yao jukwaani Ijumaa iliyopita Thai Village Masaki jijini Dar.
Uzao wa BSS Mary Lucos akipagawisha mashabiki wa Skylight Band.
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani.
Mashabiki wa Skylight Band wakionekana kupagawishwa na burudani waimbaji wa Skylight Band.
Umati wa mashabiki wa Skylight Band ukisakata rhumba ndani ya kiota cha Thai Village.
Utamu wa burudani ya Skylight Band unapowachizisha mashabiki.
Yachuma nataka mukanda ya Yachuma......Umati uliofurika Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village ukisebeneka na Style mpya ya Skylight Band.
Mashabiki walipata fursa ya kuonyesha ufundi wao katika kucheza style mpya ya Band hiyo "Yachuma chuma"
Kina dada nao walicheza ile Tiki tiki titi titti..... na mwishowe walijishindia Complimentary za kuingia bure popote pale Skylight Band inapopiga.
Hapo sasa....
Watu weweeeeeeeeee....ni balaaa njoo Ijumaa hii ujioneee uhondo wa Skylight Band.
Zoezi likaendelea na watu kujishindia Complimentary zao.
Blogger King Kif akishow love na Mh. January Makamba kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Baadhi ya vijana wakipata picha ya kumbukumbu na Role Model wao Mh.January Makamba ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
William Malecela a.k.a LEMUTUZ naye alipata Ukodak na Mh. January Makamba.
Mh. January Makamba aliyeambatana na mdogo wake Thuwein Makamba wakipata picha ya kumbukumbu na wadau pamoja na marafiki.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwa na mashabiki wake wakipata Ukodak na Mh. January Makamba. Mh. Makamba alimpa pongezi za dhati Meneja wa bendi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kutoa burudani ya muziki wa Live Band ambao unagusa rika zote na kuwataka wazidi kukaza buti zaidi kufikia anga za kimataifa.
Msanii Barnaba akipata Ukodak na Mdau Faraja wa The East African (mwenye T-shirt ya Blue) akiwa na marafiki zake.
King Kif na wadau wakipata moja moto moja baridi taratibu huku wakisikiliza mziki mzuri wa Skylight Band.