|
Utata umeendelea kuibuka kuhusu picha zinazosadikiwa ni za hivi karibuni zikimwonesha Wema Sepetu na Nasib Abdul "Diamond Platnumz" katika nyakati tofauti kwenye nchi moja huko Asia wakiwa kimahaba CHUMBANI
Picha hizi zimehusishwa na usaliti wa Diamond kwa mpenziwe wa sasa aitwaye Penny, na gazeti moja la udaku lilichapisha habari kuwa wawili hao hawapo katika hali nzuri baada ya Diamond kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Wema.
Wakati Wema akiripotiwa kuwa alikuwa China kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya sikukuu yake ya kuzaliwa, Diamond aliripotiwa kipindi hicho hicho akiwa Malaysia kwa ajili ya shughuli zake za kutumbuiza na burudani.
Swali kwa Diamond:Je umerudiana na Wema Sepetu nini kinachoendelea??
'Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana Mitandaoni na Kwenye Media tofauti kwamba mimi na Mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu ambacho sikweli na taarifa hizo za uongo uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?. Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo nanfaida',
|
SIJARUDIANA NA WEMA. Lakini jana na leo swali hilo limekuja tena kwa kasi baada ya kuonekana picha mpya za Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja katika bara la Asia ambalo bila wasiwasi ni Malaysia ambako Diamond alikuwa amekwenda kufanya show,kwa picha hizi ni wazi,Diamond na Wema walikwenda kwa pamoja,katika upande wa kujitetea Leo Diamond ameandika ujumbe akikanusha taarifa za kurudiana na Wema na kusema alikuwa akifanya movie yake mpya inayofahamika kwa jina la #TEMPTATIONS Huu ndio ujumbe wake'Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii... #TEMPTATIONS .... STAY TUNED!!!! SOON!....#DayOne #Location
NOTE;Bukobawadau blog tunakuomba wewe msomaji wetu uweze ku like ukurasa wetu mpya wa facebook kupitia link hii
https://www.facebook.com/Bukobawadau?ref=hl