Ukaguzi Manispaa ya Bukoba
CAG Bw. Ludovick Utouh Akishiriki Kuimba Wimbo wa Hamasa wa MKoa wa Kagera
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Wakiongozwa na Mstahiki Meya Anathory Amani
Pia Hawa ni Waheshimiwa Madiwani Mbele Akiwa Mheshimiwa Bigambo Kutoka Kata ya Bakoba
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Fedha ya Serikali Bw. Ludovick Utouh Akiongea na Wajumbe wa Kikao
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akiwa na Msaidizi wa CAG Bw. Edwini Rweyemamu maraBaada ya Kikao Pamoja na Mzee Samwel Rwangisa Ntambala na Mulungi Kichwabuta Diwa Viti Maalum CCM Bukoba
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Wakiongozwa na Mstahiki Meya Anathory Amani
Pia Hawa ni Waheshimiwa Madiwani Mbele Akiwa Mheshimiwa Bigambo Kutoka Kata ya Bakoba
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Fedha ya Serikali Bw. Ludovick Utouh Akiongea na Wajumbe wa Kikao
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akiwa na Msaidizi wa CAG Bw. Edwini Rweyemamu maraBaada ya Kikao Pamoja na Mzee Samwel Rwangisa Ntambala na Mulungi Kichwabuta Diwa Viti Maalum CCM Bukoba
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha
ya Serikali Bw.Ludovick Utouh amewasili mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya
Ukaguzi maalum katika Manispaa ya Bukoba ili kutafuta ufumbuzi wa kutatua mgogoro uliodumu takribani miaka
miaka miwili na kukwamisha maendeleo ya wananchi wa Manispaa hiyo.
Bw. Ludovick mara baada ya
kuwasili katika mkoa wa Kagera Septemba 30, 2013 alifanya kikao cha ufunguzi wa
Ukaguzi Maalum katika Manispaa ya Bukoba na kufafanua madhumuni ya Ukaguzi huo
ikiwa ni pamoja na ni namna gani ukaguzi
huo utafanyika.
Bw. Ludovick alisema chimbuko la
Ukaguzi Maalum lilitokana na hoja zilizojitokeza baada ya kutokea kutoelewana
baina ya Waheshimiwa Madiwan wa Manispaa ya Bukoba ambapo ilisababisha
mgawanyiko mkubwa wa makundi na
kuchangia kuzorotesha utendaji kazi wa Manispaa hiyo.
Hoja hizo kuu zikiwa ni pamoja na
kukosekana kwa uwazi kuhusu miradi ya uwekezaji ilivyopatikana, Mstahiki Meya
kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha maamuzi ya Waheshimiwa Madiwani
kupitia Baraza la Madiwani.
Akifafanua kifungu cha sheria
kinachompa mamlaka ya kufanya ukaguzi maalum Bw. Utouh alisema, “Kwa mujibu wa
kifungu cha 36 cha sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008, Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anayo mamlaka ya kufanya ukaguzi pale
atakapoona kuwa inafaa katika masuala
yanayohusiana na fedha na mali za Umma.”
Aidha Bw. Utouh alieleza kuwa
alichelewa kufika katika Manispa ya Bukoba kufanya Ukaguzi Maalum kutokana na
kukufanya maandalizi ya kutosha kabla ya ukaguzi huo ikiwemo na kuuandaa Adidu
za Rejea wakati wa kufanya ukaguzi huo ili kutenda haki katika pande zote mbili
na kuumaliza mgogoro.
Adidu za Rejea 13 za Ukaguzi
Maalum Manispaa ya Bukoba
Kuchunguza usahihi wa utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji wa
kituo cha kuosha magari (ACE Chemical
Ltd), Kuchunguza uhalali wa nyaraka na kiasi kilichowekezwa cha sh.297,000,000kwenye
mradi wa kuosha magari
Kuchunguza tatizo na sababu zilizopelekea viwanja 800 kutogawiwa
kwa wananchi waliochangia gharama za upimaji, Kuchunguza wa upimaji viwanja
5,000
Kuchunguza miradi wa ujenzi wa soko, ujenzi wa kitega uchumi na kituo cha Mabasi, ujenzi wa
chuo cha ualimu, ujenzi wa kituo cha maarifa na ujenzi wa Bwawa kwa ajilli ya
utalii.
Kuchunguza Kiwanja cha Shule ya Msingi Kiteyagwa, Barabara ya
kupitia Kagondo Kaifo hadi Kagondo Karuguru na kuchunguza masuala mengine ya matumizi
ya fedha yanayoashiria ubadhirifu.
Onyo, Bw.Utouh pia alitoa onyo kali kwa viongozi wanaolumbana
katika Manispaa ya Bukoba kutojaribu kuwarubuni wakaguzi ambao ameambatana nao
katika ukaguzi huo. “Wakaguzi hawa ni wenye ujuzi wa kutosha na wa muda mrefu
msije mkajaribu kuwapelekea vibahasha mtajisumbua bure na hawatapokea.” Alisema
Bw. Utouh.
Vilevile Bw. Utouh aliwaagiza
Katibu Tawala Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba Kuhakikisha
kuwa watendaji wote walikwishahama na watahitajika kutoa maelezo katika ukaguzi
huo maalum wapatikane ili kutoa ushirikiano wa dhati.
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian Massawe alimshukuru Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Fedha ya Serikali kufika mkoani hapa ili kutoa suruhu ya
mgogoro wa muda mrefu uliokwamisha jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wa
Manispaa ya Bukoba.
Taarifa ya ukaguzi maalum katika
Manispaa Bukoba itakamilika ndani ya siku 35 kuanzia Septemba 30, 2013 na mara
baada ya kukamilika taarifa hiyo itakabidhiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ili
kuwawajibisha wale wote watakaobainika kufuja fedha na mali za serikali na
kuuumaliza mgogoro uliodumu miaka miwili.
Imeandikwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013