Wakuu wa kampuni za simu Kenya wahojiwa
Bob Collymore ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni kubwa ya huduma za simu za mkononi Safaricom
Polisi nchini Kenya wamewahoji maafisa wakuu watendaji wa kampuni za huduma za simu za rununu kuhusu usajili wa kadi za simu za mkononi zinazotumia huduma za kampuni hizo.
Hatua ya polisi imefuatia ripoti kuwa simu zenye kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa zilitumiwa na magaidi walioshambulia jumba la Westgate mjini Nairobi wiki mbili zilizopia.
Hatua ya polisi imefuatia ripoti kuwa simu zenye kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa zilitumiwa na magaidi walioshambulia jumba la Westgate mjini Nairobi wiki mbili zilizopia.
Wanne hao walitishiwa kukamatwa mnamo siku ya Jumatatu baada ya maafisa wa serikali kuwatuhumu kwa kuuza kadi za simu ambazo hazijsajiliwa.
Hata hivyo walikana tuhuma hizo.
Mnamo mwaka 2010, serikali ya Kenya ilieleza kuwa sharti mmiliki wa simu kusajili kadi yake ya simu ya mkononi katika hatua ya serikali kuzuia visa vya uhalifu wa kutumia simu za mkononi. Hata hivyo sheria ilianza kutekelezwa mwaka jana.
Takriban watu 67 waliuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab .
Katika taarifa yao ya pamoja, maafisa hao wakuu wa kampuni za huduma za simu,Safaricom, Bharti Airtel, Orange Kenya na Yu Essar – walisema kuwa walitoa taarifa kwa polisi asubuhi ya leo.
Walikanusha madai ya kuwepo simu ambazo hazijasajiliwa na kusema kuwa wanafuata masharti yakimataifa kuhusu usalama.
Lakini kwenye mahojiano na BBC mkuu wa tume ya mawasiliano ya Kenya, Francis Wangusi alisema kuwa polisi wana ushahidi ulio kinyume na madai ya maafisa hao.
Kwamba watu wangali wanatumia kadi za simu ambazo hazijasajiliwa.
Wakenya milioni 29 wamesajili kadi zao za simu wakati wengine milioni 1.6 wanatumia kadi zisizosajiliwa.
Haya yanajiri baada ya taarifa kusema kuwa polisi wanajaribu kutafuta nambari za simu zilizotumiwa na watu waliohusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya Westgate na kusababisha vifo vya watu 67 huku mamia zaidi wakijeruhiwa.
Mnamo Jumatatu wakuu wa kampuni za huduma za simu na mawakala wao walionywa kuwa huenda wakakamatwa kwa makosa ya uhalifu na kukosa kusajili kadi za simu za wateja wao.
Waziri wa mawasiliano Fred Matiang'i alisema kuwa polisi wanafanya msako kote nchini kuwatafuta wale wanaokiuka sheria inayoshurutisha usajili wa kadi za simu iwe ni wakuu wa kampuni za simu au mawakala wao.
CHANZO;BBC