Bukobawadau

MUTUKULA NA WIZI WA MCHANA KWEUPE.

Picha: jengo la muda Mutukula linalotumika sasa kwa ukaguzi 

Tanzania tumejenga imani kuwa raia wake ni huru na  nchi inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria na 
utawala bora na  sio nchi ya kidikteta.  Mutukula hali hii ni tofauti kwa raia wake ambao  ni 
mchanganyiko wa mataifa jirani waganda,wanyarwanda, na warundi. Nilikuwa nafanya utafiti kwa nini 
waganda wamechelewa kujifunza  kuongea Kiswahili fasaha ukilinganisha na wenzao.  Jibu limejitokeza 
kuwa lugha hii ilitumiwa na askari  majambazi na wahalifu ambao walikuwa wamesheheni jeshi la  Iddi 
Amin miaka ya sabini. Hivyo wakachukulia lugha hii kuwa ni lugha ya wahalifu wasiokubalika katika jamii.
Wahalifu wa  Iddi Amin ambao mara nyingi walifanya vitendo vya uhalifu wakati wa usiku raia waliweza 
kuwatambua  kwa lugha waliyokuwa wakiitumia (ua yeye, piga yeye) lakini si kwa sura.Raia wazawa wa 
maeneo ya Mutukula na maeneo jirani wanafahamu haya yote na ni mashahidi wa kuongea 
yaliyowasibu baba zao na mama zao. Zaidi ya miaka 30 sasa tangu nyakati hizo bado kuna wizi na 
ujambazi ambao umegeukia upande wa Tanzania wala sio Uganda. Baadhi ya maafisa wa serikali 
wanatumia nyadhifa zao kudhulumu raia mizigo yao mchana kweupe na kuichukua majumbani mwao 
kwa matumizi binafsi. Juzi nilikutana na kijana Honesty Bujune(0785301912) analia kwa sababu
alinyang’anywa  boksi  la majani ya chai na Ofisa anayefanya kazi Ofisi za TRA Mutukula  kwa sababu
amekosa  hongo la shilling 10,000/= alizoamrishwa ampatie ili arudishiwe mzigo wake.Kisa ni kwamba 
alikutana naye barabarani akadai ampatie elfu kumi ili asimkamate alivyombembeleza akamtishia 
kumpeleka polisi. Na hivyo mzigo huo ukawekwa kwenye gari lake na kuupeleka  nyumbani  kwake kwa 
matumizi binafsi. Imedaiwa  kuwa sasa hivi wasafiri wengi wanadhulumiwa  vitu vyao na ofisa huyu na 
kuvipeleka nyumbani kwake kwa mtindo kama huu. Tunajua kuwa maafisa wa forodha wako Mutukula 
kwa maslahi ya Taifa na si kwa maslahi ya matumbo yao binafsi. Je huu ndio mfumo mpya ulioanzishwa 
na wenzetu wa ushuru wa forodha? Meneja wa TRA Kagera/Kamishina wa TRA wana taarifa hizi?
Usumbufu hapa Mutukula umekithiri  kutokana na Afisa kama huyu asiyejali  maadili ya kazi zake 
tunaomba serikali iliangalie hili. 
Fumbuka
Next Post Previous Post
Bukobawadau