Bukobawadau

CAMERA YETU MJINI BUKOBA IJUMAA YA LEO NOV 15,2013

Muda mchache kabla ya kung'oa nanga kuelekea Jijini Mwanza , Camera yetu ikikuangazia maeneo ya bandarini na kukutana na Meli yenye historia kubwa sana ndani ya  Manispaa yetu, ni wazi wakazi wa mkoa wa kagera wamekuwa wakipata mahitaji ya kuingia na kutoka kupitia meli hii.

Meli hii inajulikana  kama  MV Victoria,kama inavyoeleweka moja ya njia za kuingia mkoani Kagera basi maji ni njia mojawapo,meli hii inayotoa huduma ya abiria na mizigo kwa gharama nafuu inaingia na kutoka mkoani Kagera kila siku ya jumatatu,jumatano na ijumaa kama hii leo.
Ni meli ya siku nyingi na mpaka sasa bado ni tegemezi,historia inaonyesha imesafirisha watu wengi ,Wasomi wengi wanaikumbuka ambao leo ni maofisa wakubwa
Viongozi wengi ndani ya Nchi na nje wanaikumbuka kwa ujumla kipindi wanasoma mkoani hapa walitumia Meli hii kuja na kurudi makwao

Kisiwa cha Musila.
 Shughuli za uvuvi zikiendelea ndani ya ziwa victoria
Muonekano wa mlima wa Kahororo
Bukoba Club jioni ya leo
Muonekano wa Jengo la Bukoba Club

Jioni ya leo viwanja vya Bukoba Club, Mdau Jamal Kalumuna wa Jamco Production na Jamco Blog akicheck na Camera yetu 
Tukiwa bado maeneo ya Bukoba Club, Camera uso kwa uso na Ndg Mugisha maarufu kama Mugisha Video.
Maisha ya kiendelea kama kawaida katika viwanja hivi vya Bukoba Club.
Bustani safi pembezoni mwa Ziwa Victoria hakika inavutia.
Daraja la Bukoba Club kuelekea mchangani
Kulia mwa picha hii barabara inayoelekea Kiroyera Camp kuna kiwanja kiitwacho  New Paradise ama kwa hakika ni sehemu nyingine safi kwa kutulia.
Vijana wakiendelea kufurahia maji na upepo safi kutoka ziwani.
Pembezoni mwa ziwa victoria Mjini Bukoba,muonekano wa kiwanja cha SPACE BEACH MOTEL
Next Post Previous Post
Bukobawadau