DOZI A SIKU KUTOKA KWA CHRIS MAUKI
Sio mara zote katika mahusiano maneno yanayotamkwa kumaanisha kile kinacho tamkwa bali maana iliyofichwa nyuma ya maneno yaliyotamkwa, mwanaume anaweza kumaanisha kile alichotamka lakini bahati mbaya jinsia ya kike sio hivyo. Mwanamke anaweza kutamka A kumbe anamaanisha B. Kwa mfano, ndugu za mwanamke wanapokuwa wengi au wanapo kuja mara kwa mara nyumbani kwenu mwanaume anaweza kusema moja kwa moja “Naona inabidi uongee na ndugu zako waanze kupungua maana unaona watoto wetu wamekuwa na wanatakiwa kulala kwa uhuru sasa” Tofauti na mwanaume, mwanamke akitaka kufikisha ujumbe huu huu wakati ambapo ndugu za mwanaume wanakuwa wengi nyumbani kwenu yeye anaweza kusema “Mpenzi naona kama nyumba yetu inakuwa ndogo, vitu vinaongezeka, we need to do something” Sasa kama wewe kaka hujui kusoma maana iliyo nyuma ya pazia utaanza kupoteza muda wako kutafuta nyumba kubwa au kugombana na mkeo ukidhani anapenda maisha ya starehe, kumbe kaka unafikishiwa ujumbe tu kuwa punguza ukoo wenu hapo nyumbani. “Guys lets not read the lines but between the lines” - Chris Mauki.