Bukobawadau

JIJINI MWANZA RAIS KIKWETE ALIPOKEA KOMBE LA DUNIA LEO nov 29,2013

Rais Jakaya Kikwete amepokea rasmi Kombe la Dunia katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza mapema jioni hii. Aiita ziara ya Kombe mkoani humo “jambo la kihistoria.”
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua na kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo
Katika uwanja wa ndege jijini Mwanza wadau na viongozi wa TFF wakiwa tayari kulipokea kombe la dunia.
Vilevile, JK amesisitiza kuwa ziara hiyo ni “deni” la kimichezo ambalo Tanzania lazima ililipe kwa kukuza vipaji vya soka nchini humu, ili siku moja iweze kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuwania hilo Kombe la Dunia.

Taswira ya mapokezi ya kombe la dunia Jijini Mwanza ikiwa ni kwa mara ya kwanza nchini katika ardhi ya mwanza kabla ya kuendelea jijini Dar es Salaam.
Next Post Previous Post
Bukobawadau