Bukobawadau

MAJAMBAZI YAENDELEZA OPERATION HUKO BIHARAMULO NI BAAADA YA OPERESHENI KIMBUNGA YA JK

Hali imekuwa tete kwa siku ya jana kuanzia majira ya saa 2 Asubuhi na saa kumi na moja jioni katika kata ya Lusahunga Nyakahura  mpaka meneo ya  Murusagamba Wilaya ya Biharamulo.
Watu wapatao kumi 10 wanasaidikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za kali(Bunduki aina ya smg)mapanga, fimbo na marungu wameteka magari 15 na kupora vitu mbalimbali zikiwemo fedha ambazo thamani yake haijafahamika na kuwa jeruhi  baadhi ya watu  wilayani Biharamulo Mkoani Kagera
Mmoja wa majeruhi ambaye amelazwa katika Hospitali teule  ya wilaya ya Biharamulo Bw.Gideon Chango amesema tukio lililomkuta limetokea  Novemba 21  majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Busiri kata ya Lusahunga, wakati wakielekea katika mnada wa Ng'ombe.
Madereva wa magari makubwa madogo, Semi , fuso pamoja na abiria walipata wakati mgumu baada ya kupigwa, kudhalilishwa na kuumizwa.
Mmoja wa wadau kutoka Mjini Bukoba Ndg Romward Bashemela amekutwa na mkasa huo pamoja pamoja na kuchukuliwa hela nyingi alizokuwa nazo.


Kumeendelea kuwa na patashika mitaa ya Nyakahura mzani baada ya madereva wengi walionusurika kuonelea pale ndio sehemu sahihi kujipozea.
Mnyetishaji mmoja anasema ;Magari yamepigwa Risasa, Fuso moja imepigwa tairi ya mbele ikapinduka, Semi moja baada ya kupigwa tairi ya mbele ikabidi atembelee rim ili kujiokoa na mtiti huo wa majambazi.
Polisi wamefanya jitihada kadri ya uwezo wao ingawa ni wachache kwa kulinganisha na eneo husika hivyo wanazidiwa.

Kaimu Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Mwapati amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba msako mkali unaendelea dhidi ya majambazi hayo yaliyokimbilia porini baada ya uharifu huo.
Kupitia mtandao huu wa Bukobawadau , Wadau wanaiomba serikali iangalie swala hili kwa jicho la tatu ili kuhakikisha Watanzania waliopo maeneo haya wanaishi kwa amani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau