SOKO LA SENENE LEO NOV 23,2013 MJINI BUKOBA
Pamoja na wingi wa senene kwa siku ya leo, bado swala zima la uchumi kwa wadau ni tatizo lililopelekea senene hao kudoda.
Senene ni kitoweo asa mkoani Kagera,Zipo aina nyingi za wadudu ambao katika baadhi ya makabila hapa nchini hutumiwa kama kitoweo na pia katika uzalishaji wa bidhaa za vyakula kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Lakini senene ambao hupatikana kwa wingi mwishoni mwa kila mwaka kama hii leo,japo kutokana na mabadiriko ya kimazingira kwa sasa senene wana msimu maharumu..wanaweza kutoka kila baada ya miezi mitatu.Senene ni miongoni mwa wadudu wanaotumiwa zaidi na kabila la Wahaya mkoani Kagera kama kitoweo, pengine kuliko kabila jingine unalolifahamu.
Hao ndio senene wa Tsh500 kwenye mfuko.
Ni full hekaheka mwanzo mwisho.
Ili kufanywa kitoweo,wadudu hawa jamii ya panzi au nzige hukamatwa, kuondolewa mbawa, miguu, papasi na mikia yake kisha kukaangwa kwa mafuta au hata bila mafuta. Katika hatua hii huwa tayari kwa kuliwa na chakula chochote ambacho huwa kimeandaliwa.
Haya ni magunia yenye senene, mpaka kufikia saa 9 alasiri hali ilikuwa hivi sokoni
Lakini si wakati wote senene hawa huandaliwa kwa njia hii, kwani wakati mwingine wingi wao husababisha wale wanaowakamata kushindwa kuwatengeneza. Inapofikia hatua hii senene hawa huchemshwa katika maji kwenye sufuria kubwa na baada ya muda huondolewa na kukaushwa kwa kuwekwa kwenye chanja juu ya moto. Chanja hii inajulika kwa jina la kihaya 'olushero'.
Mara nyingi senene wanaokaushwa, huifadhiwa kwa lengo ya kutumika kama kitoweo kwa familia husika na zaidi hutumwa kama zawadi ya heshima kwa wapendwa wa familia hizo, hasa wanaoishi mbali ambako si rahisi kupatikana.
Gharama sio kuwanunua Senene au kuwapata?....gharama kubwa ni kuwatengeneza ,kuwamenya, kuwaandaa kama hivi unavyo jionea kupitia bukobowadau blog
Hakika senene leo wamezua balaa kila kona ya mji
Fungu moja kwenye mfuko limeuzwa kwa Tsh500,hadi kufia saa moja jioni limeuzwa kwa Tsh100.
Kuanzia soko la senene lilipo mpaka mtaa wa Migeyo hali ipo hivi