ULAZAJI NA UUNGANISHAJI BOMBA LA GESI ASILIA WAKAMILIKA KWA KM 142
Uunganishaji na ulazaji wa bomba la gesi asilia kutoka mtwara hadi jijini Dar-es-salaam,umekamilika kwa kilometa 142 kati ya kilometa 542 za bomba hilo,huku wakandarasi wakiunganisha bomba hilo kwa kilometa nne kwa siku vikiwa vikosi kazi sita.
Meneja wa ubora na viwango ambaye pia ni msiamizi wa mradi huo Bwana Peter Erasmusi,ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa mradi huo uliofanywa na wajumbe wa ushirikiano wa kimaendelo toka mataifa mbalimbali duniani, wanaochangia miradi ya kitaifa ya maendeleo,walipotembela mradi huo ili kujionea maendeleo yake.
Katibu mkuu ya nishati na madini Bwana Eliakimu Chacha Maswi,amewaomba watanzania kuwaunga mkono kwa kutoa ushirikiano kwenye mradi huo,huku akidai kuwa kukamilika kwa mradi huo wa ulazaji wa bomba la gesi asilia,utakuwa mwarobaini wa tatizo la kukatika kwa umeme nchini na nchi kuelekea katika uchumi mkubwa.